Leo katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika ikulu chamwino, Raisi Dkt. Samia Suluhu ameeleza nia ya dhati ya kuunga mkono mapendekezo ya WHO kuanzisha vitengo vya kuhudumia watoto.
Katika mkutano huo akiwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus Amesema Tanzania inaunga mkono mapendekezo hayo ya WHO kuanzisha vitengo maalumu vya kuhudumia watoto hususa ni wale wanaozaliwa kabla ya wakati Hadi sasa kufikia asilimia thelasini ya vituo vinavyotoa huduma
Aidha Rais Dkt. Samia Alieleza kuwa Tanzania iko katika mchakato wa kutimiza lengo la kufikisha huduma za afya kwa watu wote (UHC), dira inayotekelezwa tangu kupitishwa kwa Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote wa mwaka 2023.
Lakini pia alieleza juu ya ugonjwa wa Marburg ambapo, Rais Dkt. Samia amesema kufuatia tetesi za uwepo wa ugonjwa huo Mkoani Kagera, Serikali ilichukua hatua za kuwafanyia uchunguzi watu waliodhaniwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo kwa kushirikiana na wataalamu wa afya katika maeneo hayo na tarehe 11 Januari ikatuma timu maalumu ya dharura.
Vilevile alianisha kwamba ugonjwa wa Marburg ni mara ya pili kutokea kwa virusi hivyo nchini Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza mlipuko wa virusi hivyo ulitokea mwezi Machi mwaka 2023 mkoani Kagera.
Na alimalizia kwa kusema Tanzania ni nchi salama kwa sasa na Iko salama na kiwakaribisha wageni kufanya shughuli za kibiashara pamoja na shughuli zingine