Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa leo kwenye mkutano wa CCM Dodoma ameweka wazi sababu za CCM kushinda chaguzi mambimbali nchini.
Ameyasema hayo akihutubia kwenye siku ya pili ya mkutano huo na kueleza sababu za kukubalika na kuaminika kwa chama cha mapinduzi.
“Awamu zote za uongozi jamhuri ya muungano wa Tanzania na Zanzibar zimesimamia kwa ukamilifu utekelezajiwa sera na ilani ya chama cha mapinduzi na zimetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu hii ndiyo sababu katika kipindi chose CCM imekuwa ikiaminiwa, ikikubalika na kutekeleza sera zake kwa watanzania na kupelekea ushindi katika chaguzi hapa nchini” Amesema.
Aidha ameeleza juu ya ziara alizofanya pamoja na mawaziri na wakuu wa mikoa kutembelea miradi na kushuhudia shukrani kutoka kwa wananchi juu ya miradi hiyo.
“Mimi pamoja na mawaziri wennzi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya tumefanya ziara kote nchini kupita kutembelea miradi kukutana na wananchi tumeshuhudia faraja na shukrani na pongezi kwako kutoka kwa watanzania” Amesema.
Pia amemshukuru mwenyekiti wa chama cha mapinduzi na Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kupeperusha vyema benders ya chama vizuri.
Vilevile ameeleza juu ya kazi nzuri za Raisi wa Tanzania bara Dkt. Samia Suluhu na na raisi wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwamba ni sababu ya taifa kujizolea umaarufu na sifa nzuri kimataifa