Chama cha mapinduzi CCM baada ya kipindi kifupi kukaa bila makamu mwenyekiti wa chama kupitia katiba yao kimemtambulisha Ndg. STEVEN MASATU WASIRA kuwa makamu mwenyekiti wa CCM.
Ni baada ya kukidhi vigezo kutokana na wasifu wake katika siasa na chama lakini pia uzalendo katika taifa na kukubali demokrasia na muungano wa pande mbili kati ya Zanzibar na Tanzania bara.
Wasira ni mingoni mwa makada wa chama cha mapinduzi waaminifu na mzalendo pia, ambae katika utumishi wake wote katika chama cha mapinduzi alihudumu vyema na hata aliwahi kuwa miongoni mwa walio wahi kuunda baraza la mawaziri nchini.
Tufungue kidogo kabati la Ndugu wasira.
Historia kwa ufupi.
Stephen Wasira alizaliwa mwaka 1945 katika Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara (ana miaka 70). Alisoma katika shule tatu tofauti, ya kwanza ni Shule ya Msingi Bariri 1956-1959, ya pili ni Shule ya Msingi Nyambitilwa 1960–1961 na kisha akamalizia Shule ya Msingi Kisangwa mwaka 1962 – 1963.
Kati ya mwaka 1964–1967, Wasira alisoma elimu ya Sekondari katika Chuo cha Ukufunzi Uingereza (British Tutorial College) na kuhitimu kidato cha nne.
Wakati anasoma sekondari (1965–1967), pia alifanya kazi akiwa msaidizi wa masuala ya maendeleo ya jamii na alipohitimu kidato cha nne alianza kuitumikia Tanu akiwa katibu wa wilaya mwaka 1967-1973.
Mwaka 1975–1982 alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na mwaka 1982 akateuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Washington, D.C. Alipokuwa huko alisoma na kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Uchumi na Uhusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Amerika (American University) kilichopo Washington DC mwaka 1982–1985.
Wasira alisoma Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Umma kati ya mwaka 1985–1986 na aliporejea nchini kuendelea na utumishi wa uwakilishi wa wananchi, aliteuliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani mwaka 1990-1991.
Kati ya mwaka 1993–1995 alisoma tena Shahada ya Uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Amerika.
Ndani ya chama chake CCM, amekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) tangu mwaka 2007 na mwaka 2012 akachaguliwa katika wadhifa huo na tena kwa kura nyingi kuwashinda wajumbe wote wa Tanzania Bara.
Lakini pia amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2011 na tena 2013 na sasa ni makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.