Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye mkutano mkuu wa CCM, Dodoma amewakumbusha wajumbe na wanachama wa CCM kwenye mkutano mkuu dhamira yao kubwa kwa mustakabali wa chama na taifa
Aidha amewata watimize wajibu wao waliopewa na katiba chama kwa uadilifu, uzalendo, na kuwazia kesho ya Tanzania.
Vilevile aliwashukuru wajumbe na kuwapongeza baada ya ushindi mkubwa wa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika 2024.
“nitumie fursa hii kukushukuruni na kuwapongeza kwa ushindi mkubwa tulio upata”Amesema.
Lakini waliwakimbusha juu ya mwaka wa uchaguzi 2025 wawe wamoja zaidi ili wakamilishe maandalizi ya uchaguzi.
“Mwaka huu wa 2025 ni mwaka wa uchaguzi mkuu tunawajibika kutoka hapa tukiwa wamoja zaidi ili tukakamilishe aandalizi ya ushindi wetu 2025” Amesema.
Pia alieleza wajibu huo watautekeleza kwa kushinda uchaguzi na kutoa uongozi Bora Tanzania.
Na alimalizia kwa kuwasihii wanachama na wajumbe kupambana na watu wanaotaka kuwarudisha nyuma kwa kulinda heshima waliopewa na wananchi.
“Tupambane nao kulinda heshima tuliyopewa na wananchi katika kuliongoza taifa letu” Amesema
