Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hasan kupitia mkutano mkuu wa chama uliofanyika jijini Dodoma amekemea siasa za mapema kwa wagombea.
Aidha ameeleza wameshapata malalamiko na ushahidi wa picha za watu wanaofanya misafara ya kwenda majimboni na wanaoitisha mikutano mikuu ya majimbo kwa visingizio vya shughuli za kiserekalilakini wakiwa na dhamira ya kujitambulisha kwa wanachama.
Vilevile akaainisha kwamba wana ushahidi wa picha nyingi sana hivyo anatoa onyo mapema ili kukemea hilo.
“masuala ya kampeni za mapema tunayakemea tayari tayari tumeshapata malalamiko lakini na ushahidi wa picha kwa watu wanaofanya misafara kwenda majimboni, watu wanaoitisha mikutano mikuu ya majimbo kwa visingizio vya ufugaji au mambo mengine lakini dhamira ni kujitambulisha kwa wanachama sasa tunaomba Tutoe onyo mapema sana”.
