Tangu kocha Ruben Amorim apewe jukumu la kuismamia Manchester united, ni kama vile imekuwa kheri kwa Amad, amekuwa akimpa nafasi katika mechi kadha wa kadha, na bahati nzuri kila anapopewa nafasi anaonyesha kile ambacho mwalimu anategemea kwa asilimia nyingi.

Nafikiri sasa amaenza kujenga imani katika mioyo ya mashabiki wa Manchester United.
Ukikumbuka michezo kadhaa amekuwa akiibuka shujaa
Mechi dhidi ya Mahasim wao, wanatokea nyuma Bruno anasawazisha Amad anafunga kazi ✍️ Tayari hapo aliipatia timu yake point 3 muhimu🙌🎯
Mech dhidi ya Liverpool tena Anfield, wakati ambao Liverpool wanaamini washamliza kazi, Amad anakuja kuwashangaza dakika 80′ anaipa timu yake point moja ya maan.

Mechi ya jana dhidi ya Southampton 🔥🔥
Pengine mashabiki wengi walishakata tamaa kutokana na kile kilichokuwa kinaendelea mpka dakk 80
Anatokeea huko alikotoka anapiga Hat- trick ya maan Come back ya kwenda🔥
82’⚽
90’⚽
90+4′ ⚽
🔥🔥🔥
Amad Diallo nimchezaji pekee kutoka Afrika ambaye amendika rekodi kubwa kwa mechi chache tuu tangu aaminiwe na kocha Amorim.
Yeye mwenyew anasema hivi,
“Nataka kuwa hapa Man United kwa muda mrefu,…hata maisha yangu yote!
Nina furaha kucheza beki wa kulia, no10 au popote pale ambapo meneja ataniweka… nataka kupigania klabu hii!”. Amad

Anakua Mchezaji wa kwanza wa Kiafrika kufunga hat-trick ya PL kwa Manchester United katika historia ya klabu.
Mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwa Manchester United tangu Cristiano Ronaldo alipoondoka mwaka 2022.
Kumbuka kuwa Mechi dhidi ya Southampton mabao yote amefunga ndani ya dakk 10.
