RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibad Dkt Hussein Ali Mwinyi wamepongezwa kwa juhudi zao za makusudi kukuza utalii katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli ya kuwapongeza viongozi hao imetolewa na Waziri Balozi Dkt. Chana ambaye amesema kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamefanya kazi kubwa ya kuinua na kuitangaza sekta ya Maliasli na Utalii kupitia Filamu ya The Royal Tour, hivyo ni mashirikiano ya wataalam wa pande zote mbili yataendeleza jitihaza hizo.
“Ni wazi kuwa programu ya The Royal Rour imekuwa na matokeo chanya katika sekta ya utalii kwa pande zote mbili za Muungano kutokana na idadi ya watalii walioongeza tangu kuzinduliwa kwake pamoja na kuongezeka kwa wawekezaji walionesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania”. Amesema Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana.
Naye Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai M. Said licha ya kuwapongeza wataalam wa pande mbili za Serikali ya Muungano kwa kuamua kukutana, amewataka kuhakikisha wanaimarisha mashirikiano katika kutangaza vivutio vya Utalii vya pande zote mbili (SMT na SMZ) ili kuongeza idadi ya watalii kwenye vivutio vya Utalii nchini.