UKWELI usiopingika kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amechukua hatua kadhaa katika kuhakikisha nishati safi na salama inapatikana na kufanikisha maendeleo ya sekta hii nchini.
Chini ya uongozi wake, Tanzania imekuwa ikifanya juhudi za kusambaza umeme vijijini, kuhimiza matumizi ya nishati mbadala, na kutekeleza miradi ya nishati safi.
Kwa mfano, imekuwa na uhamasishaji wa matumizi ya nishati mbadala kama vile gesi na umeme kwa kupikia, na miradi ya ujenzi wa mabwawa ya umeme na uzalishaji wa gesi.
Aidha, kuna juhudi za kuunganisha kaya zote na gridi ya umeme ya taifa na kutoa mitungi ya gesi bure kwa kina mama na kaya masikini ili kuepuka matumizi ya kuni na mkaa ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira na madhara ya afya.
Hii inaonyesha nia ya kuhakikisha nishati inapatikana kwa wingi na ni ya aina ambayo haichafuzi mazingira.
Dhamira yake ilionekana, alipozindua mkakati wa taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kuhakikisha kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2033.
Rais Dkt. Samia anataka kuwepo nguvu ya pamoja kuanzia wahisani wa kimaendeleo, taasisi za umma na sekta binafsiPicha: Presidential Press Service Tanzania
Matangazo
Hatua hiyo inakuja miezi michache baada ya kiongozi huyo kuongoza mkakati kwa nchi za Afrika kuwawezesha wanawake barani humu kuanza kutumia nishati safi ya kupikia, wakati aliposhiriki Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) huko Dubai.
Ndani ya mkakati huo ambao ni wa miaka 10, Rais Dkt. Samia anataka kuwepo nguvu ya pamoja kuanzia wahisani wa kimaendeleo, taasisi za umma na sekta binafsi ili kuongeza chachu kufikia malengo yake:
Ikiwa sehemu ya kushajiisha uzinduzi wa mkakati wenyewe, makundi mbali mbali ya watu wamehudhuria wakiwamo viongozi wa kisiasa, kidini, wanadiplomasia pamoja na makundi mengine kama vile madereva wa malori, mamalishe na vikundi vingine vya wanawake ambao wanatajwa kuwa sehemu kubwa ya matumizi ya nishati isiyo rafiki.
Zaidi ya asilimia 90 ya kaya nchini Tanzania hutegemea nishati chafu itokanayo na kuni, mkaa pamoja na mabaki ya kinyesi cha wanyama kwa ajili ya kupikia na shughuli nyingine za majumbani, hali ambayo wataalamu wanaonya kwamba imekuwa sehemu ya ongezeko la matatizo ya kiafya kwa wengi huku pia uharibifu wa mazingira ukivunja rekodi.
Ili kutoa mkazo kuhusu mkakati huo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imeanisha vipaumbele vitakavyozingatiwa kuanzia ngazi ya kaya mpaka taifa.
Ripoti zinaonyesha kwamba kila mwaka nchini Tanzania watu 33,000 hupoteza maisha kutokana na mikasa inayosababishwa na matumizi ya nishati isiyo salama, na kiwango hicho kinadhihiri zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uwepo wa nishati safi na salama ya kupikia bado ni ndogo.