Wanaosadiskika kuwa Wachambaji madini haramu 100 kwenye mgodi wa dhahabu usiofanya kazi Afrika Kusini wafariki baada ya kunasa chini ya mgodi huo kwa miezi kadhaa huku polisi wakijaribu kuwaondoa .
Msemaji wa jamii zilizo athiriwa na uchimbaji madini anaefahamika kama Sebelo Mnguni, akizungumza na shirika la habari la Associated Press aliliambia kwamba simu ya mkononi iliyotumwa juu ya mgodi huo na baadhi ya wachimba migodi walio okolewa siku ya ijumaa, ilikuwa na video zilizokuwa zikionyeaha miili kadhaa iliyofunikwa kwa plastiki chini ya ardhi.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0008.jpg)
Aidha ameweka wazi kwamba takribani watu 100 walifariki katika mgodi pale polisi walipoanza operesheni mwezi Novemba kuwalazimisha wachimba migodi waondoke.
“Takribani watu 100 walifariki katika mgodi katika mkoa wa kaskazini magharibi ambako polisi walianzisha operesheni mwezi Novemba kuwalazimisha wachimba migodi kuondoka” alisema Sebelo.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0009.jpg)
Aliongeza kwa kusema Wanashuku watu hao walikufa kwa njaa kwasababu ya kukosa maji kwani serikali ilizuia huduma za vyakula na maji kupelekwa katika eneo Hilo kwasababu shughuli zilizokua zinaendelea ziko kinyume na Sheria na kuanza operesheni ya kuwaondoa.
Jeshi la polisi kupitia Msemaji wake Brigedia Sebata Mkngwabone alisema bado uchumguzi taarifa kujua miili mingapi iliyopatikana na ni manusura wangapi walio okolewa baada ya operesheni ya uokoaji Kuanzishwa jumatatu.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0010.jpg)