⚪️ Manchester United wamemuongeza Nene Dorgeles winga mwenye umrinwa miaka 22 kutokea Mali 🇲🇱 kwenye orodha ya wachezaji wanao wahitaji kwenye majira ya baridi, Kijana huyo raia wa Mali anaekipiga kwenye timu ya RB Salzburg.
Manchester United wanaendelea kuonyesha nia ya kumuhitaji huku wakiwa wanazungumza kwa kina na kufata matakwa ya klabu na mchezaji kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.
⚪️ Manchester city wamekubaliana na Palmeiras juu ya dili la kunasa saini ya mlinzi wakati Victor Reis mwenye umri wa miaka 18 anaekipiga kwenye klabu ya soka ya palmeiras
Makubaliano ya mdomo mpaka sasa na palmeiras ni uhamisho wa kinda huyo utakuwa ada yake ni chini ya €40.
⚪️ Mlinzi wa kati kutoka katika taifa la ufaransa anekipiga katika klabu ya Chelsea Axel Disasi anatarajia kuondoka katika viunga vya Chelsea kama ataendelea kuwa nje ya kikosi.
Baada ya Chukwuemeka, Cesarea Casadei, Senator Veiga, Ben Chilwell kupanga kuondoka pia Disasi amepanga hivyohivyo.
⚪️ Klabu ya Napoli kutokea nchini Italy imefikia makubaliano na Paris saint-Germany juu ya dili la uhamisho wa Kvaratskhelia.
Makubaliano ya mdomo ni kwamba kiungo huyo atahamia Paris kwa ada ya zaidi ya €70m huku Kvaratskhelia akihitaji mkataba mrefu wa miaka mitano.