Nifahari kushuhudia unakua na mwanamke anaekupa heshima ya kuitwa baba kwa kukuzalia mtoto, ila simulizi ya Beckham imekuwa tofauti, hii hapa hemu tuone nini alifanya.
Kabla David Beckham hajamuoa Victoria, siku moja Victoria alirudi kwa Beckham akiwa analia na anaomba waachane, Beckham alijitahidi kuongea nae lakini hakufanikiwa, Beckham alishangaa tatizo ni nini? Mbona hajakosea chochote na anamuonyesha mapenzi makubwa lakini Victoria anataka waachane?
Beckham alijipa muda mambo yatulie kwanza na baadae alimtafuta Victoria ili amuulize tatizo ni nini au kuna kitu kamkosea? Kweli walikutana na Victoria akamueleza Beckham kuwa hakuna chochote alichomkosea ila alienda kwa daktari na akagundulika ni Infertility yani hana uwezo wa kubeba mimba hivyo akamuomba Bekham atafute mwanamke mwingine.
Licha ya kuelezwa hivyo lakini David Beckham hakujali alipiga goti moja na akamuomba Victoria amkubalie kuwa mke wake, Victoria alishindwa kuzuia machozi yake na akakubali ombi la David Beckham kweli jamaa alimuoa kisha miujiza ya kweli ikatokea licha ya kuwa Doctor alitabiri kuwa Victoria hana uwezo wa kubeba mimba lakini Victoria alipata mimba na wakapata mtoto wao wa kwanza wakamuita Brooklyn.
Wakawa na furaha isiyo na mipaka na leo hii wana watoto wanne, siku moja Beckham alihojiwa kuhusiana na mapito haya na akajibu kwa kusema “Kama ningeondoa mapenzi yangu kwa mwanamke niliempenda wakati wa matatizo, ningepoteza amani ya moyo wangu”
Ni miaka 25 imepita tangu waoane na bado wapo pamoja, siku zote upendo wa kweli huwa unashinda wakati wa matatizo.
Je! Wewe ungeweza alichofanya Beckham?