Tamaduni, Mila na Desturi ni vitu vinavyo tuongoza kuwa watu wema na wenye ubinadamu, lakini baadhi ya tamaduni hazibebi taswira ya ubinadamu bali hubeba taswira ya ukatili.Ipo tamaduni ya kupunguza matiti huko magharibi mwa Afrika ambayo husababisha maumivu makali na kufanya wanawake kukosa amani.
Wanaotekeleza hilo hudai kwamba hatua ya kuzuia kukua kwa matiti ya wasichana wanaoanza kubaleghe huwazuia wasichana wadogo kuwavutia wanaume na hivyo basi kuepuka dhuluma za kimapenzi lakini jambo hilo limetajwa na wanaharakati kama ukiukaji wa haki za wasichana na dhuluma za kijinsia .
Jiwe hutiwa katika moto kama kaaa kisha kupitishwa juu ya matiti kwa lengo la kuyapunguza. Je! ni tamaduni Gani unadhani katika eneo lako itokomezwe?