Anaandika Godbless Lema kupitia Ukurasa wake Wa X
“CCM wanatufuatilia sana, wana hifadhi kila kauli zetu juu ya wagombea wetu wote ktk mchakato wa uchaguzi wa Chama wa viongozi wakuu Mwezi January , bila shaka watazitumia kauli hizi Mwaka 2025 kama tutashiriki na kutakuwepo na uchaguzi huru. Lakini pia wananchi wana share kila habari inayoleta fitina na uchungu miongoni mwetu. Hii ni hatari.
Chama cha siasa za upinzani na harakati za kutafuta utawala bora zinaongozwa na inner purpose na passion , kusudi likifa Chama kinakufa kwa sababu 99% ya viongozi na wanachama wanafanya wajibu wa kazi za Chama kwa kujitolea , sasa watawezaje kujitolea kama hakuna purpose ? Moral inajengwa na nidhamu .
Kwa hali ilivyo sasa tuna uchungu sisi kwa sisi kuliko tulivyo na uchungu dhidi ya CCM , kampeni ya sasa ya dhihaka na matusi kwa viongozi na wananchi ambao hatuwaungi mkono imekuwa kali kuliko kampeni ya kukomesha mauaji na utekaji Nchini.
Let’s get back to the purpose na kila mtu aheshimiwe na kuthaminiwa kwa upande aliouchagua kwa maana ndiyo demokrasi yenyewe”