– Mabilioni ya pesa yakwamishwa makusudi na wajanja wachache mahakamani
– utaratibu ni kila anayeshindwa kulipa mkopo hukimbilia mahakamani kuweka zuio la dhamana zake zisifidie mikopo
– wakopaji wanachezesha kesi zinachukua miaka na miaka kusikilizwa hadi kuisha
– zipo kesi zimekaa miaka 5, nyingine 7 na nyingine hadi miaka 10
– zipo nyingine kila inapoitwa ina ahirishwa tena kwa muda mrefu
– michezo hiyo inasababisha uchumi wa wananchi na wafanyabiashara wema kudumaa, mabenki kukwama kutoa mikopo
– JAMVI LA HABARI kuzidi kufichua hatua kwa hatua jinsi ‘wahuni’ wanavyojitajirisha kupitia mikopo
– wapo wanaojificha kwenye vivuli vya michezo, wengine dini na wengine siasa
————
*_” Wengi wao ukiwaona huwezi kuwadhania kama wanafanya uhuni wa namna hiyo, wapo wanaojificha kwenye vivuli vya michezo, wengine wanajipachika karibu na viongozi wa kiserikali na usiombee siku moja apige picha na kiongozi atakavyoisambaza hiyo picha kuonyesha kuwa yeye ni rafiki wa kiongozi husika kumbe magirini tu…wapo wengine wanajifanya waumini wazuri wa dini na kwenye nyumba za ibada hukaa mbele na inapotokea michango huchanga kwa mamilioni na wanaombewa kabisa kumbe masikini ya Mungu ni pesa za haramu zinazotokana na kudhulumu akiba za watu, Ni mambo ya aibu aisee”. Ameongeza Kihampa_ **
Na. Mwandishi wetu,
Mabilioni ya pesa ambayo yangeweza kukopeshwa kwa wafanyabiashara wa ngazi mbalimbali ikiwemo wajasiliamali wadogo yamekwamishwa makusudi mahakamani na wafanyabiashara wakubwa na wakati wanaokopa kiasi kikubwa cha pesa na kukataa kulipa kwa kukimbilia mahakamani kufungua kesi za aina mbalimbali pindi taasisi zilizowakopesha zinapotaka kuokoa mkopo walioutoa kwa wafanyabiashara hao
Orodha ya wafanyabiashara hao ambao wanadaiwa kutumia mbinu mbalimbali kukwepa kurejesha mikopo yao gazeti hili imeendelea kuipata na wengi kati yao ni watu wanao onekana kuheshimika sana katika jamii wengine wakiwa ama waliwahi kuwa katika nyadhifa maeneo mbalimbali kama vile michezoni huku wengine wakijiweka makwapani mwa wanasiasa wakubwa nchini
Taarifa zinasema kuwa katika kufanikisha michezo hiyo, utaratibu ni kila anayeshindwa kulipa mkopo hukimbilia mahakamani kuweka zuio la dhamana zake zisitumiwe na taasisi za mikopo kufidia mikopo waliyochukua
Ndio kusema kwamba wakopaji wengi hutumia ujanja wa kuwa wanachezesha kesi zinachukua miaka na miaka kusikilizwa hadi kuisha huku taasisi za mikopo zikiendelea kupata hasara na wafanyabiashara wengine kushindwa kupata mikopo
“zipo kesi zimekaa miaka 5, nyingine 7 na nyingine hadi miaka 10 na kuna kesi zinafunguliwa hadi zinajifia zenyewe haziishagi, watu sio waaminifu. Wanatumia watu wachache wasio waaminifu kuchezesha michezo hii. Mwisho wa siku wanaoathirika ni wenye akiba zao katika mabenki”. Ananukuliwa Jessy Kihampa
“zipo nyingine kila inapoitwa ina ahirishwa tena kwa muda mrefu
michezo hiyo inasababisha uchumi wa wananchi na wafanyabiashara wema kudumaa, mabenki kukwama kutoa mikopo na ndio maana vita dhidi ya vijana kujikwamua na umasikini inakuwa ngumu kwa sababu hizo”. Anaongeza na kusisitiza
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa wapo wafanyabiashara wanaoshindwa kweli kurejesha mikopo na kwenda mahakamani kwa nia njema ya kutafuta namna ya kusogeza muda mbele ili wajipange kulipa deni lakini wengi hukimbilia mahakamani kutumia haki yao ya kikatiba kwenda kufanya kitu kinachoitwa ‘Kupaki’ kesi na kuendelea kufanya mambo yao bila ya kujali madhara wanayoyasababisha
Katika kadhia hii, JAMVI LA HABARI litqendelea kuzidi kufichua hatua kwa hatua za jinsi gani ‘wahuni’ hao wanavyojitajirisha kupitia mikopo hiyo na huku mitaani kupita na kutamba
” wengi wa wanaokopa na kukataa kulipa sio kwamba hawana uwezo wa kulipa, ni kwamba wanafanya makusudi na ndio maana wenyewe wanaita kuzipaki kesi mahakamani, wanafungua kesi leo inakuja kuhukumiwa baada ya miaka 8 huko mbele”. Amesisitiza Kihampa
Ameaongeza kuwa wafanyabiashara wanaojinufaisha kiharamia wanatumia maarifa makubwa ikiwemo wengine kujiweka karibu na viongozi wakubwa wa serikali, wengine kujihusisha na vilabu vikunwa vya michezo huku wengine wakijionyesha kuwa ni waumini wazuri wa dini na kwamba wana mcha Mungu haswa na inapotokea michango katika taasisi za dini hutoa kwa mamilioni
” Wengi wao ukiwaona huwezi kuwadhania kama wanafanya uhuni wa namna hiyo, wapo wanaojificha kwenye vivuli vya michezo, wengine wanajipachika karibu na viongozi wa kiserikali na usiombee siku moja apige picha na kiongozi atakavyoisambaza hiyo picha kuonyesha kuwa yeye ni rafiki wa kiongozi husika kumbe magirini tu…wapo wengine wanajifanya waumini wazuri wa dini na kwenye nyumba za ibada hukaa mbele na inapotokea michango huchanga kwa mamilioni na wanaombewa kabisa kumbe masikini ya Mungu ni pesa za haramu zinazotokana na kudhulumu akiba za watu, Ni mambo ya aibu aisee”. Ameongeza Kihampa
Endelea kufuatilia gazeti