– Ni kutokana na Usimamizi duni wa dhamana zilizowekwa na wakopaji wa Benki ya Biashara Tanzania na Benki ya Azania kwa mikopo iliyotolewa
– Watoa mikopo ya mabilioni ya shilingi bila kuwekewa dhamana na wakopaji, wengine dhamana zao hazijahakikiwa wala bima kuhuishwa
– Ni maandalizi ya utengenezaji wa mikopo chechefu
Na. Mwandishi wetu,
Wakati jamii ikiendelea kujiuliza ni kwa namna gani mikopo chechefu imekuwa ikishamiri kila siku nchini, baadhi ya benki hasa zinazomilikiwa na serikali zimeibua mapya kutokana na kutoa mikopo ya mabilioni bila kuwekewa dhamana na wakopaji wa fedha hizoTaarifa ua mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali nchini-CAG inaitaja benki ya biashara kufanya uzembe huo huku ikihatarisha fedha za wananchi ambazo zimewekezwa kama mtaji‘’Benki ya Biashara Tanzania ilitoa mkopo wa shilingi bilioni 6.56 kwa wateja sita ambao hawakuweka dhamana kama inavyotakiwa na vipengele vya mikataba ya mikopo yao. Pia, Benki ilitoa mikopo mingine ya shilingi bilioni 5.50 kwa wateja wawili bila kuhuisha dhamana zao za awali kabla ya kupata mkopo mwingine’’.imenukuliwa taarifa ya CAG ‘’Vilevile, nilibaini kutokuwapo kwa ripoti za uthamini za dhamana zilizoahidiwa za wateja sita zilizohusisha shilingi bilioni 8.34 kinyume na Muongozo wa ukopeshaji’’. imeongezaTaarifa hiyo imesema Pia, ‘’mapitio yangu yalibaini kuwa taarifa za dhamana za Benki ya Azania zilizotumika katika kukokotoa makadilio ya matarajio ya hasara inayotokana na kutokukusanya madai, zilibaini kutokuwepo kwa nyaraka kama vile ripoti za uthamini na bima za mikopo zinazohusisha mikopo ya shilingi bilioni 383.22 iliyotolewa kwa wakopaji wapatao 60’’. AmeongezaCAG anasema kuwa hati za dhamana zisizotosheleza zinaweza kusababisha hatari ya benki kushindwa kurejesha mkopo kwa kunadi dhamana zilizowekwa endepo wakopaji watashindwa kurejesha mikopo yao.
Ninapendekeza Benki ya Azania na Benki ya Biashara Tanzania kuhakikisha mikopo iliyotolewa ina dhaminiwa na dhamana ya kutosha na yenye ubora pamoja na kuimarisha udhibiti wa usimamizi wa mikopo iliyotolewa ikiwa ni pamoja na kufuatilia mikopo iliyotolewa ikuungwa mkono na dhamana. Jana gazeti hili liliripoti kuwa mikopo isiyolipika maarufu kama MIKOPO CHECHEFU inaelezwa kuwa moja ya kikwazo kikubwa cha ufanisi wa benki nyingi nchini na kichocheo kikubwa cha kurudisha nyuma uwiano wa kiasi cha fedha katika mzunguko wa jamii kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kuwa mikononi mwa watu wachache hasa wafanyabiashara wakubwa na matajiri ambao wameibua mchezo mpya wa kukopa mabilioni ya shilingi na kukataa kulipaTaarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali kuhusiana na mikopo chechefu aliyoitoa mwezi machi mwaka huu inaonyesha ni kwa namna gazi benki zinazomilikiwa na serikali zinavyojikongoja kwa kukosa mtaji kutokana na sehemu kubwa ya mtaji wake kuwa mikononi mwa wakopaji waliokataa kulipa na hivyo kuifanya serikali kuunganisha baadhi ya benki ili kuunsda benki nyingine zenye mtaji mkubvwaKatika taarifa hiyo CAG anaeleza kuwa alikagua utendaji wa benki zinazomilikiwa na Serikali, mifuko ya hifadhi ya jamii, Shirika la Bima la Taifa, na taasisi zinazohusika na usimamizi wa masoko ya mitaji na dhamana nchini Tanzania.‘
‘’Nilibainisha maeneo kadhaa ambayo taasisi hizi zina mapungufu ya kiutendaji na zinahitaji maboresho ili kuhakikisha utendaji wao unakuwa bora.Kwa benki tatu zinazomilikiwa na Serikali ambazo ni, Benki ya Maendeleo ya TIB, Benki ya Azania na Benki ya Biashara Tanzania nimebaini mapungufu kadhaa kama vile kutosimamia ipasavyo kwa mikopo, na kutokidhi matakwa ya udhibiti.’’. Inasema taarifa hiyo ya CAGMikopo chechefu, na Benki zinazopata hasara‘’Ukaguzi wangu ulibaini Benki ya Maendeleo ya TIB iliendelea kupatahasara kabla ya kodi, mwaka 2023 hasara ilifikia shilingi bilioni 5.92(2022: hasara kabla ya kodi ilikuwa shilingi bilioni 131.97). Wakati Benki ya Biashara Tanzania ilipata hasara kabla ya kodi ya shilingi bilioni 41.40 (2022 faida kabla ya kodi shilingi bilioni 6.87),ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 48.27 sawa na asilimia 703. Hasara hii ilichangiwa zaidina kufutwa kwa mikopo chechefu iliyorithiwa kutoka iliyokuwa Benki ya TIB Corporate’’.inaongeza taarifa hiyo ya CAGTaarifa hiyo inasisitiza kuwa katika mapitio ya mikopo chechefu ilibaini kuwa Benki ya Maendeleo ya TIB ilikuwa na mikopo chechefu ya asilimia 21.50 kufikia tarehe 31 Desemba 2023 (2022: mikopo chechefu asilimia 20.28), wakati Benki ya Azania ilikuwa na mikopo chechefu asilimia 7.44 hadi kufikia 31 Desemba 2023 ( 2022: mikopo chechefu asilimia 18.25). kinyume kabisa na matakwa ya kanuni inayosimamia ukomo wa mikopo ya BOT‘’Pamoja na kupungua kwa uwiano wa mikopo chechefu kutoka mwaka uliopita kwa Benki ya Azania, ni vyema kutambua kuwa benki zote mbili bado zilivuka kiwango kinachokubalika na kilichowekwa na Benki Kuu ya Tanzania cha asilimia 5. Pia, Benki ya Maendeleo ya TIB na Benki ya Azania kwa pamoja zilikuwa na mikopo chechefu ipatayo shilingi bilioni 206.04 (2022 mikopo chechefu shilingi bilioni 262.72) ikiwa imepungua kwa shilingi bilioni 56.68 huku sababu ikiwa ni kutozwa kwa mikopo chechefu ‘’ Imeongeza
CAG amebainisha kuwa Kuna uwezekano wa kuzorota kwa ubora wa mtaji wa mkopo kunaharibu mtaji mkuu wa Benki na unaathiri uwiano wa utoshelevu wa mtaji na utendaji wa benki hizo.
Ambapo katika hoja hizo amependekeza Serikali ichukue hatua za haraka kushughulikia masuala yanayozikabili benki hizi, ikiwa ni pamoja na kuongeza mtaji kwa Benki ya Maendeleo ya TIB, kuboresha udhibiti wa gharama na kupunguza uwiano wa mikopo chechefu hadi kufikia kiwango kinachokubalika cha asilimia 5.
Hayo yanajiri wakati mdhibiti na mkaguzi huo akionyesha wasiwasi juu ya ufanisi wa benki za Serikali kwenye Usimamizi duni wa dhamana zilizowekwa na wakopaji wa Benki ya Biashara Tanzania na Benki ya Azania kwa mikopo iliyotolewa ya shilingi bilioni 403.62
Soma hapa sehemu ya taarifa hiyo ya CAG
Benki ya Biashara Tanzania ilitoa mkopo wa shilingi bilioni 6.56 kwa wateja sita ambao hawakuweka dhamana kama inavyotakiwa na vipengele vya mikataba ya mikopo yao.
Pia, Benki ilitoa mikopo mingine ya shilingi bilioni 5.50 kwa wateja wawili bila kuhuisha dhamana zao za awali kabla ya kupata mkopo mwingine. Vilevile, nilibaini kutokuwapo kwa ripoti za uthamini za dhamana zilizoahidiwa za wateja sita zilizohusisha shilingi bilioni 8.34 kinyume na Muongozo wa ukopeshaji.