Inbox
MALEZI BORA NI NGUZO YA MAADILI KWA WATOTO.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwalinda na kuwalea watoto katika malezi mema ili kujenga kizazi bora na chenye maadili ambacho kitafuata mila na desturi la taifa letu
Hayo yalisemwa na Polisi Kata ya Hezya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Jaqueline Shumbi Juni 11, 2024 wakati akitoa elimu ya umuhimu wa malezi bora kwa wananchi wa kata hiyo na kuelezea malezi bora ya mtoto yanatokana na mzazi/mlezi anapomfundisha mtoto yale yote yaliyo mema ambayo yatamjenga katika maadili na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
Sambamba na hilo, Mkaguzi Shumbi amewataka wazazi hao kuwajenga watoto wao katika misingi ya imani ya dini zao kwa kwenda nao kwenye nyumba za ibada ili katika makuzi yao wawe na hofu ya Mungu na kutenda yaliyomema katika maisha yao ya kila siku.