HAKUNA SAFARI ILIYOBORA ZAIDI YA USALAMA WAKO
Polisi kata wa kata ya Iyula iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoa Songwe Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Yakobo Dungumara amewataka abiria kujali usalama wao kwanza na kutoa taarifa kwa madereva wasiofuata sheria za usalama ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Kauli hiyo ilitolewa Juni 10,2024 alipokuwa anatembea barabara ya Iyula kuelekea Mnada wa Idiwili na kukutana na abiria wakiwa wamepanda gari kwa njia ya hatari na kutoa elimu kwa abiria hao hasa madhara ya kupanda kwenye gari la mizigo ambayo ni kinyume na sheria pia ni hatari kwa usalama wao
Aidha, Mkaguzi Dungumaro amewataka abiria hao kuacha tabia ya kukaa juu ya bomba za gari kwa usalama wao na watoe taarifa kwa madereva wazembe ambao awafuati sheria za usalama barabarani ili wachukuliwe hatua za kisheria.