- Mahakama ya Rufaa chini ya Majaji Rehema Mkuye, Abraham Mwampashi na Zainab Muruke yafutilia mbali hukumu ya Mahakama kuu divisheni ya biashara iliyoipa ushindi kampuni ya State Oil dhidi ya benki ya Equity
- State Oil walikopa Dola milioni 18 za kimarekani sawa wastani wa Shilingi bilioni 45 za Kitanzania kwa kampuni ya Dubai wakidhaminiwa na benki hiyo iliyotoa ‘Special Letter of Credit’
- Ikatumia mkopo huo kufuta madeni yao katika mabenki mengine yaliyokuwa yanawadai na kiasi kingine kuongezea mtaji
- Ulipofika wakati wa kulipa ikakataa kulipa mkopeshaji akambana mdhamini na kutumia ‘Special Letter of Credit’ aliyoweka kulipwa mabilioni aliyokopesha
- Mkopeshswaji alipofatwa na mdhamini aliyelipishwa mabilioni kwa niaba yake akakataa kulipa na kukimbilia mahakamani na Jaji Magoiga akampa ushindi katika hukumu iliyojaa utata
- Mahakama ya Rufaa sasa yaagiza shauri hilo lianze kusikilizwa upya katika Mahakam ya Biashara
- Kwa hukumu hiyo sasa benki inaweza kuendelea na taratibu za kurejesha amana yake kutokana na dhamana zilzowekwa na kampuni hiyo
- Wanufaika wengine wa Mikopo chechefu waliokopa na kukimbilia mahakamani sasa matumbo joto, wahaha kujisafisha bila mafanikio
- Jamvi la Habari lapongezwa kusimama kidete kufichua madudu yaliyofanywa na ‘ushirika chechefu’ ya kukataa kulipa mikopo kutumia Mahakama
Na. Mwandishi wetu,
Mahakama ya Rufaa imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama kuu divisheni ya biashara katika moja ya kesi maarufu za mikopo chechefu baina ya kampuni ya State Oil dhidi ya Benki ya Equity kesi ambayo Mahakama Kuu hiyo chini ya Jaji Magoiga iliipa ushindi kampuni ya husika ambayo ilikopa dola milioni 18 (zaidi ya Shilingi Bilioni 45 za kitanzania) na kukataa kulipa kisha kukimbilia mahakamani
Ikiongozwa na majaji watatu Rehema Mkuye, Abraham Mwampashi na Zainab Muruke mahakama hiyo imeona kasoro kadhaa za kiuendeshaji wa kesi katika mahakama kuu divisheni ya biashara iliyofunguliwa na kampuni ya State Oil ikitaka mahakama itoe amri kwa kampuni hiyo kutokulipa kiasi cha shilingi bilioni 45 za kitanzania ilizokopa kwa kampuni ya Lamar ya Dubai na kudhaminiwa na benki ya Equty
Katika hukumu hiyo ambayo gazeti hili imepata nakala yake, majaji hao wanasema kuwa wametumia mamlaka waliyopewa kisheria ya kufuta hukumu na mwenendo mzima wa kesi hiyo na kuelekeza ianze kusikilizwa upya katika mahakama kuu divisheni ya biashara huku ikionyesha makosa kadhaa kubwa likiwa ni kutokushirikishwa kwa upande muhimu katika shauri hilo la Equity Benki ya Kenya
‘’Kiasi cha mkopo cha USD 18,640.000.00 kilitolewa na LAMAR kwa SOT(State Oil Tanzania) kupitia akaunti ya escrow iliyofunguliwa na EBK (Equity Bank Kenya) kwa jina lake. Baada ya hapo, EBK ililipa deni lote la SOT kwa EBT na benki zingine. EBK pia ilijilipa kamisheni ya USD 372,800.00 yenyewe, USD 750,000.00 kwa NISK kwa huduma za ushauri na udalali na USD 74,560.00 kwa serikali ya Kenya kama ushuru wa bidhaa na Salio lililosalia kwa SOT lilikuwa USD 736,899.74.’’ Inasomeka sehemu ya Hukumu hiyo
Inaelezwa kwamba hati ya madai ya mjibu maombi Katika shauri la Msingi Mahakama Kuu haikufanyiwa marekebisho baada ya Mahakamu Kuu kutoa uamuzi wa kuunganisha EBK kuwa sehemu ya kesi baada ya EBK kuwa sehemu ya kesi Jaji aliyesikiliza shauri alijielekeza isivyo kwa kushindwa kutoa amri ya mleta Madai SOT kufanya marekebisho ya hati yake ya Madai ili kuweza kuunganisha Madai dhidi ya EBK kwa minajili ya haki.
Hata hivyo Mawakili wa pande zote hawakuona kama ilikuwa ni Makosa makubwa kwa Mahakama kuu kushindwa kutoa amri ya marekebisho ya Hati ya Madai.
Mahakama ya Rufaani kwa mamlaka yake yenyewe imeona kuwa Mahakama kuu ilifanya makosa makubwa kwa kushindwa kutoa amri ya kurekebisha Hati ya Madai baada ya EBK kuunganishwa kwenye Shauri sambamba na kuamua kuwa hati ya Madai irekebishwe huku ikiwa imefuta hukumu na amri za mahakama kuu na kuagiza kesi isikilizwe upya na hakuna gharama kwa pande zote.
Kwa mujibu wa Sheria ya mamlaka ya mahakama ya Rufaan Tanzania Act 141 iliyofanyiwa marekebisho 2019 kifungu cha 4(2) inaipa mamlaka mahakama ya rufaan kutumia mamlaka yake kufanya mapitio kwenye uamuzi wa mahakama na kuona kama mwenendo na Hukumu vilifuata sheria kama sivyo wanamamlaka ya kufuta mwenendo na Hukumu na kutoa amri Shauri au kesi kuanza upya.
‘’madhumuni ya uamuzi huu, mambo ya msingi yafuatayo kutoka ambayo suala lililotolewa hapo juu linatokea, inatosha: Mkata rufaa wa 1, Equity Bank Tanzania Limited (EBT) ilikuwa imepanua huduma nyingi za benki kwa mhojiwa, State Oil Tanzania Limited (SOT) ambazo zilidhaminiwa na aidadi ya mali zisizohamishika, hati fungani na dhamana kwa ajili ya
EBT. Wakati mwingine mnamo 2018, kwa nia ya kutafuta njia za kulipa deni lake
sio tu kwa EBT lakini pia kwa benki zingine nchini Tanzania ambazo ni; Benki ya FNB, TIB
Benki na Benki ya ABC, na pia kwa mtaji wa ziada wa kufanya kazi, SOT ililazimika kutafuta
na kupata mkopo kutoka kwa mkopeshaji wa ufadhili wa kigeni. Kwa kusudi hilo, EBK ilikuwa alikaribia na kupitia hilo, mshauri wa kifedha aitwaye Nisk Capital Advisors of
Nairobi (NISK) ilijishughulisha na ushauri wake wa kifedha na udalali
huduma, SOT ilifanikiwa kupata mkopo wa nje wa USD 18,637,500.00. kutoka
Lamar Commodity Trading DMCC ya Dubai (LAMAR) inayolipwa baada ya miezi 12.’’ Inasomeka zaidi hukumu hiyo
Hukumu inaeleza zaidi kuwa kwa kuzingatia asili ya mgogoro kati ya wahusika na kiasi cha fedha kinachohusika kuwa kikubwa, hitaji la kesi ya haki ambayo ni kwa mujibu wa utaratibu wa lazima sheria, ni kitu ambacho hakiwezi kuhujumiwa katika kesi ya papo hapo, sivyo tu suala la vyama kutobaguana bali ni kwa maslahi pia ya haki ambayo sheria za taratibu za lazima zinafuatwa.
Taarifa kuhusu suala hilo zinaonyesha kuwa kampuni ya State Oil ilikopa Dola milioni 18 za kimarekani sawa wastani wa Shilingi bilioni 45 za Kitanzania kwa kampuni ya LAMAR ya Dubai wakidhaminiwa na benki hiyo iliyotoa ‘Special Letter of Credit’
Ambapo state Oil Ikatumia mkopo huo kufuta madeni yao katika mabenki mengine yaliyokuwa yanawadai na kiasi kingine kuongezea mtaji na ulipofika wakati wa kulipa ikakataa kulipa mkopeshaji akambana mdhamini na kutumia ‘Special Letter of Credit’ aliyoweka kulipwa mabilioni aliyokopesha
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mkopeshswaji alipofatwa na mdhamini aliyelipishwa mabilioni kwa niaba yake akakataa kulipa na kukimbilia mahakamani na Jaji Magoiga akampa ushindi katika hukumu iliyojaa utata
Hivyo basi, kutolewa kwa hukumu hiyo sasa benki inaweza kuendelea na taratibu za kurejesha amana yake kutokana na dhamana zilzowekwa na kampuni hiyo na kuwafanya nanufaika wengine wa Mikopo chechefu waliokopa na kukimbilia mahakamani sasa matumbo joto, wahaha kujisafisha bila mafanikio
Jamvi la Habari lapongezwa kusimama kidete kufichua madudu yaliyofanywa na ‘ushirika chechefu’ ya kukataa kulipa mikopo kutumia Mahakama
Aidha gazeti hili lilipata kuripoti kuwa Jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukaribisha na kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchini unaelezwa kutiwa kigingi na tabia chafu inayozidi kuota mizizi ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kushirikiana na baadhi ya majaji wa mahakama kuu wasio waaminifu kuyatapeli mabenki ya ndani na nje ya nchi kwa na hivyo kuwanyima fursa wafanyabiashara wadogo na wakati kushindwa kuaminiwa na kupata mikopo.
Orodha ya wafanyabiashara wanaotumia mahakama kutapeli na kudhulumu mabenki iliyofanyiwa uchunguzi na kuthibitishwa na gazeti hili, inaonyesha kuwa wengi kati ya wafanyabiashara hao wanajihusisha na biashara za Mafuta na ushafirishaji ambapo wastani wa shilingi za kitanzania Trilioni 1.3 wamekopa katika benki mbalimbali za ndani nan je ya nchi na kukataa kulipa kisha kukimbilia mahakamani ambako pia wanadaiwa kupata ushindi kwa njia zisizo za kawaida
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wafanyabiashara hao wanaoheshimika nchini wakionekana machoni mwa watu kuwa ni matajiri na wengine wakijionyesha kama wacha Mungu na wenye kumuogopa Mungu huku wengine wakijinasibu kama wana michezo na wawekezaji wakubwa wanaitumia mahakama hasa mahakama ya biashara kama kichaka chao cha kufanyia uhalifu huo wa kimkakati
‘’hebu fikiria, mtu amekwenda TADP amekopa bilioni 40, akaenda Azania benki akakopa bilioni 70, hajaishia hapo akaenda Equity benki akakopa bilioni 110, halafu akapanda ndege hadi ujerumani akavidanganya baadhi ya viwanda vya huko kuwa anaenda kuwekeza mafuta Kahama, nako wakamkopesha mali na mtaji wa zaidi ya bilioni 220, halafu anakataa kulipa mkopo makusudi kwa kukimbilia Mahakamani na Jaji anampa ushindi bila kuzingatia Ushahidi na ukweli kuwa hizo bilioni 220 za ndani na bilioni 220 alizochukua ujerumani zote kwa pamoja zinaingia kwenye deni la Taifa na kukataa kwake kulipa mkopo kunatunyima fursa sisi wafanyabiashara wadogo kuaminiwa’’. Anasema Christopher Kabison mfanyabiashara wa vifaa vya simu Kariakoo
Kabison anaongeza kuwa kama Serikali haitachukua hatua za haraka kuingilia kati hali hii basi jitihada za Rais kutaka mabenki yakopeshe wafanyabiashara kwa riba nafuu zitabaki kuwa ndoto kwani hakuna benki itakayokuwa tayari kuendelea kupoteza mitaji yake huku mahakama zinazotarajiwa kuwa ni sehemu ya haki zikitumika kuhalalisha uchafu huo
‘’juzi nilikuwa napitia hukumu za mahakama, nimeshuhudia jaji mmoja amempa ushindi Stati oili ambaye alikopa dola milioini 26 equiti benki halafu akakataa kulipa, ukizipitia hizi hukumu unaweza ukajiuliza kama jaji wakati anatoa hukumu alikuwa sawa sawa ama ameonja kidogo..na jaji huyo huyo akahukumu hukumu kama hiyo kwa kampuni ya derina ambayo ilikopa zaidi ya bilioni 40 na kukataa kulipa. Sasa hapa tukisema mahakama inatumika kuhalalisha ujambazi dhidi ya watanzania tutakuwa tumeionea’’. Aliongeza Kobisoni
Kwa mujibu wa taarifa na nyaraka ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa miongoni mwa makampuni yanayoongoza kufilisi mabenki huku wakitumia mahaka ni pamoja na KOM GROUP ambayo imeweka kibindoni zaidi ya bilioni 440 na kukataa kulipa na kuziacha solemba benki za TADB,AZANIA pamoja na EQUITY sambamba na ujerumani
Wengine wanaoongoza genge la kukwamisha jitihada za Rais Dkt. Samia katika kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kukataa kulipa mikopo na kisha kukimbilia mahakamani na mahakama kuwapa hukumu za ushindi ni pamoja na kampuni ya TSN iliyozidhulumu benki za NMB na Equity, Derina Group iliyozidhulumu benki za CRDB na KCB huku BIG BON ikitajwa kuidhulumu benki ya NBC kama ambavyo Masasi construction inavyopambana kuidhulumu benki ya Equity kwa kutumia mahakama
Sambamba na kampuni hizo, nyingine ni Global Agency, State Oil inayomilikwa na Nilesh Suchak kama ilivyo kwa NAS HAULIERS na Continental reliable zinazotamba kuwadhulumu CRDB, NMB, NBC,EQUITY, KCB na nyinginezo
Ikiwa kitendo hiki cha wafanyabiashara hawa wakubwa kukopa na kuacha kulipa madeni kisha kukimbilia mahakamani na mahakama kuwapa ushindi kitaachwa kuendelee kuota mizizi kitapelekea Taifa kuwa na kikundi ‘GANG’ cha wafanyabiashara wanaoutawala Uchumi wa nchi na hivyo kuhatarisha amani ya Taifa
Kuwepo nje ya mzunguko wa benki hizi mabilioni hayo ya shilingi ni kiashiria kibaya katika ukuzaji wa Uchumi huku Gavana wa benki kuu akiombwa kuchukua hatua za haraka kuingilia sintofahamu hii inayozidi kushika kasi
‘’kama BOT hawatakuwa serious na kuingilia kati kunusuru hili jambo, benki zitafungwa hizi, ama zisipofungwa basi Uchumi utahama kutoka kuwa rasmi na kuwa Uchumi wa kihuni unaondeshwa na wahuni, lazima benki kuu iingilie kati haraka’’. Alisema Juma Hamad mchambuzi wa masuala ya kiuchumi
Aliongeza kuwa katika Taifa lolote ambalo linaheshimu utawala wa sheria, ni nadra kwa wafanyabiashara kukopa halafu kukataa kulipa makusudi kisa tu kuna mahakama, hali hii inaweza kushawishi na wafanyabiashara wadogo nao kukataa kulipa na ikiwa wakashindwa mahakamani basi itasababisha hali ya sintofahamu
Gazeti hili linaendelea na jitihada za kuwatafuta wote waliotajwa kukapua mabilioni hayo na kukataa kulipa huku simu zao za mkononi zikiita bila kupokelewa.