MTANDAO MPANA
Wakati vijana wa kitanzania, kina mama na walemavu wakishangilia kurejeshwa kwa mikopo ya asilimia 10 ya Halimashauri mikopo ambayo hapo awali walikuwa wakikopeswa kwa vikundi vikundi ili kujikimu na Maisha kwa kushindwa kukopeshwa na mabeki kwa kinachoitwa kukosekana kwa vigezo vya kukopesheka, imebainika kuwa mabilioni yanayotafunwa na wafanyabiashara wanaokopa benki na kukataa kulipa wakitumia mahakama mchakato wake unaratibiwa na mtandao mpana nchini
Hii ni kusema kuwa mtandao unaotumika kusuka mikopo inayotolewa na mabenki ya ndani nan je ya nchi na kisha kukataliwa kulipwa na wafanyabiashara ambao kwa kiasi kikubwa wanaheshimik na kuaminika kama ni miongoni mwa watu matajiri zaidi nchini ni mpana na unahusisha watu wengi wenye nafasi tofauti Jamvi la Habari linaweza kuthibitisha
Miongoni mwa watu wanaotajwa kuhusishwa na mitandao hiyo ni pamoja na watumishi wa mabenki wasio waaminifu ambao hutumika kuandaa makosa ya kisheria makusudi ili kutengeneza mazingira ya mkopaji kutokulipa mkopo husika na hatimaye kukimbilia mahakamani huku wanasheria wakitajwa kuhusika kurahisisha na kuandaa mazingira hayio ya dhuluma wengine ni watendaji wa mahakama na wafanyabiashara wenyewe wanaotajwa kujilipua
Taarifa zinaeleza kuwa Benki hupangiwa kudhulumiwa kwanza kabla hata mkopo husika haujasainiwa kisha wahusika wote walioshiriki kufanikisha mpango huo wanagawana mgao
Wakati gazeti hili likendelea kuripoti juu ya Sakata la wafanyabiashara kuchukua mikopo katika mabenki na kukataa kulipa makusudi, Orodha ya mabenki na makampuni waliokopa mikopo na kukataa kurejesha kisha kukimbilia mahaamani yaendelea kuvuja na kulifikia gazeti
Taarifa zinasema kuwa kampuni za UKOD OIL ,Oil com, Dar Lux, Uhuru height, Sumry Buses, Chobbo Investments na Global Agency zachota zaidi ya bilioni 200 Stanbic, CRDB,EXIM, na NCBA huku wakopaji waliokacha madeni wanatamba kumiliki magari ya kifahari na apartments zinazotokana na pesa za dhuruma
Inaelezwa kuwa kampuni ya Ukod oil international imekopa na kulitekeleza deni la shilingi bilioni 25 kwa benki ya Stanbic wakati Global Agency wao wakiitapeli CRDB kiasi cha bilioni 26 sambamba na Abla Apartment walioidhulumu benki hiyo bilioni 13 huku uhuru height wakipiga shere Exim benki kiasi cha dola milioni 25
Wengine ni kampuni yam abasi ya Sumry iliyoichabanga CRDB bilioni 11 na kuingia mitini huku Dar Lux yenyewe ikiibia benki ya NCBA bilioni 19 wakati chobbo investment ikitafuna bila huruma bilioni 12
Aidha muda mchache kabla gazeti Kwenda mtamboni imeonekana ikisambazwa kwa nguvu na wafuasi wa wanufaika wa mikopo chechefu video fupi ikimuonyesha wakili maarufu wa mikopo chechefu Frank Mwalongo akijichanganya mbele ya waandishi wa habari
Video hiyo imemuonyesha mwalongo ama kwa kujua au kutokujua akiwavua nguo wateja wake, akiivua nguo mahakama na majaji sambamba na kuiingiza benki kuu ya Tanzania katika Ushahidi wa uharamia wa kisheria alioufanya
‘’tumeshangaa metuita waandishi wa habari na badala ya kueleza vya maana amejikuta akijikanyaga kanyaga akikiri kufanikisha dhuluma hizo dhidi ya benki akisingizia sheria huku akihusisha Benki kuu ya Tanzania kubariki akisema BOT imewakataza wadaiwa kulipa madeni waliyokopa kwa kuwa hayajasajiliwa’’. Amenukuliwa mmoja ya waandishi waliohudhuri amkutano wake
Ameongeza kuwa Utetezi wake waibua maswali mengi kuliko majibu, wadau wahoji inakuwaje wakili mwenye akili timamu aongee bila weledi kiasi kileni kana kwamba amethibitisha kuwa ni kweli wateja wangu wamechukua pesa lakini hawajarudisha kwa sababu mahakama imeamuru hivyo
Jana, kazeti hili lilieleza kuwa
Ikiwa ni siku moja tangu gazeti hili liripoti kuhusiana na mchezo mchafu unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa wanaokopa mabilioni ya pes ana kisha kukataa kulipa makusudi fedha hizo na kukimbilia mahakamani ambako hulalamikiwa kupewa ushindi kwa njama siri zaidi zimevuja kuhusiana na mmoja wa majaji aliyetoa hukumu tata kwa wafanyabiashara wawili kupewa ushindi kwa kesi mbili za benki mbili tofauti huku wakiwakilishwa na wakili mmoja na hukumu zao zikifanana kuhamishwa kutoka kuwa miongoni mwa majaji wa mahakama kuu divisheni ya biashara na kupelekwa katika moja ya mikoa ya nyanda za juu kusini akiendelea kuwa jaji
Taarifa zaidi zinasema kuwa wakati jaji huyo akihamishwa, wafanyabiashara walionufaika na hukumu za jaji huyo na majaji wengine tajikuta wakiingia kizimbani tena kuanzia leo kusikiliza rufaa zilizowasilishwa dhidi yao kutokana na mabenki waliyoyadhulumu kukata rufaa kupinga maamuzi yaliyopelekea kuhamishwa kwa baadhi ya majaji
Taarifa za uhakika zilizoshuhudiwa katika notisi ya kesi zinazotarajiwa kusikilizwa mahakama ya rufaa ni kuwa leo Aprili 23 mbele ya majaji watatu waheshimiwa jaji Mkuye, mheshimiwa jaji Mwampashi na mheshimiwa jaji Muruke kutasikilizwa kesi ya madai baina ya ebnki ya Equity dhidi ya kampuni ya State Oil kesi ambayo inataraji kuvuta hisia za wengi kutokana na mmiliki wa kampuni hiyo bwana Nilesh kutamba mitaani kuwa amewaweka majaji mfukoni kwako sambamba na baadhi ya wanasiasa na kwamba hakuna wa kumfanya lolote hapa nchini kwa sasa
Aidha mbele ya majaji hao hao jumatatu ijayo tarehe 29 itasikilizwa kesi nyingine ya rufaa baina ya benki ya Exim dhidi ya THEM & five B huku jumanne ya tarehe 30 mbele tena ya majaji hao hao kesi nyingine ya madai baina ya benki ya Equity itasikilizwa dhidi ya kampuni ya usafirishaji ya NAS HAULIERS
Taarifa za kuanza kusikilizwa kwa kesi hizi za rufaa kwa mwezi huu wan ne na kuendelea tena mwezi wa tano kwa makampuni mengine ambayo yamefanya na kupitia mchezo kama huo zinatajwa kuwatia hofu baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wanajiaminisha kuwa mahakama ndio sehemu yao ya Kwenda kufanya chochote bila woga wowote wakitumia udhaifu wa baadhi ya majaji
MJADALA WAPAMBA MOTO
Wakati gazeti hili likiripoti kuhusiana najambo hilo, mjadala umeibuka maeneo mbalimbali nchini hasa katika mitandao ya kijamii huku mmoja wa watumiaji wa mtandao wa X zamani Twitter Martin Maranja Masese akiibua masuala kadhaa yaliyovutia wasomaji na wachangiaji maelfu kwa maelfu
Soma hapa alichokiandika Martin
“MICHEZO HARAMU KATIKA MIKOPO CHECHEFU”
Machi 2023, Rais Samia Suluhu Hassan aligusia ‘mikopo chechefu’ wakati akipokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2021/2022. Wengi hawakufahamu ni kitu gani.
Pia, nafikiri hata Rais mwenyewe wakati anazungumza hayo hakupewa taarifa vizuri na wasaidizi wake kwamba hata private banks pia zinateseka kwa kiwango cha kutisha na hii mikopo chechefu.
Tangu kupatikana kwa uhuru, madeni chechefu yamekuwa ni changamoto kwenye sekta zinazotoa huduma za fedha nchini jambo linalosababisha taasisi nyingi za kifedha kushindwa kukua kwa mitaji.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa mwaka 2020, kiwango cha madeni chechefu kilikuwa ni 9.42% tofauti ya 9.58% kwa mwaka 2019. Kiwango cha juu kuliko kinachoruhusiwa cha 5%
Akiwa, Mkurugenzi Mtendaji CRDB, Dk. Charles Kimei alisema kutengwa kwa zaidi ya TZS 150 bilioni kwa ajili ya mikopo chechefu kuliathiri kwa namna moja au nyingine upatikanaji wa faida wa benki hiyo.
Kilichoathiri faida, CRDB waliweka tengo kubwa la mikopo iliyochechefuka, CRDB walitenga TZS 153 bilioni kwa mikopo chechefu kama wasingetenga wangepata faida ya zaidi ya TZS 200 bilioni
Wafanyabiashara wazito wanadhulumu fedha za mabenki kwa kutumia mahakama. Wanachota akiba ya fedha za wateja. Wanagoma kulipa fedha hizo. Wanakimbilia mahakamani. Mahakama zinabariki.
Mchezo huo umekuwa ukifanywa na aina tatu za kampuni; (1) kampuni za mafuta (oil companies) (2) kampuni za usafirishaji (logistics companies) (3) kampuni za kilimo (agricultural companies)
Katika utawala wa awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, kampuni nyingi zinazofanya huo mchezo, zilifilisika na kukimbia nje ya nchi. Kampuni nyingine zilishtakiwa na wakurugenzi wake kufungwa.
Wanakopa moja kwa moja ndani ya nchi kisha kutengeneza mgogoro na kugoma kulipa kukimbilia mahakamani na kupewa ushindi wa kesi (BIG BON na NBC deni la TZS 22 bilioni, KOM na TADB na AZANIA)
Wanakopa kwa kampuni za kimataifa zinazojihusisha na mikopo ya kimataifa kufanikisha biashara za kimataifa na kitaifa (hudhaminiwa katika makampuni hayo na benki za ndani kwa kupewa Letter of Credit)
Ni barua kutoka benki inayohakikisha malipo ya mnunuzi kwa muuzaji yatapokelewa kwa wakati na kiasi sahihi. Ikiwa mnunuzi hawezi kufanya malipo, benki italipa kiasi kamili au kilichosalia cha ununuzi.
Kwa maana nyingine, ni ahadi ya kimkataba ya benki ya mnunuzi wa kigeni kulipa mara tu msafirishaji anasafirisha bidhaa na kuwasilisha hati zinazohitajika kwa benki ya msafirishaji kama uthibitisho.
Letters of Credit, zinawalinda exporters na importers, kupata biashara na wateja wapya katika masoko ya nje. Msafirishaji anapata hakikisho la malipo huku akimpa muagizaji masharti ya malipo yanayofaa.
Kampuni inakuwa haina uwezo wa kukopeshwa pesa au bidhaa inayouza, hivyo huishirikisha benki ya ndani kutoa udhamini kwa taasisi za kimataifa kwa kutumia (letter of credit) hupatiwa huduma husika
Kwa kuwa dhamana ya mikopo hiyo ni benki, wafanyabiashara hawa hawarudishi mikopo ya watu na hivyo taasisi za kimataifa kuzifanya benki zilizotoa dhamana kuwalipa fedha hizo. BoT wanafahamu.
Benki hulazimika kulipa mikopo hii kisheria na pindi wanaporudi kwa waliowapa udhamini kwa kutumia letter of credit wanakimbilia mahakamani na huko hupewa hukumu za ushindi (hukumu zinazofanana).
Kitu cha kushangaza sana pia, wafanyabiashara wote hawa wanahudumiwa na wakili mmoja tu maarufu kwa kesi za hivyo hapa nchini, anaitwa FRANK MWALONGO. Ni wakili wa mahakama kuu.
Kampuni zote ambazo zime’ default mikopo katika bank za EQUITY, CRDB, NMB, STANBIC wanatumia kampuni ya APPEX ATTORNEYS na mahakamani wanawakilishwa na Wakili Frank Mwalongo.
Hapa chini nitakupa orodha ya kampuni zilizofanya uhuni huo na kiasi cha fedha ambacho kimechuliwa. Mikopo ya aina hii ndiyo ile mikopo chechefu ambayo inahusika kupandisha deni la TAIFA.
KOM (Kahama Oil Mills Limited); (mali ya MHOJA NKWABI KABALO). KOM wamechukua TZS 40 bilioni Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na kugoma kulipa kwa kukimbilia mahakamani,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Development Bank – TADB) benki ya wakulima, ilianzishwa chini ya Sheria ya Kampuni, 2002 CAP 212 mnamo Septemba 2012.
KAHAMA OIL MILLS LIMITED wamechukua kutoka AZANIA BANK kiasi cha TZS 70 billion , huku wakichukua TZS 110 bilioni kutoka EQUITY BANK na kukataa kulipa zote kisha kukimbilia mahakamani.
TSN Group (mali ya Farouq Baghoza), kampuni inadaiwa TZS 8 bilioni na kampuni ya mafuta ya HASH ENERGY ambazo imekataa kulipa. Pia imechukua NMB BANK kiasi cha TZS 15 bilioni na kugoma kulipa
TSN Group imekopa TZS 80 bilioni EQUITY BANK katika utaratibu wa kudhaminiwa na letter of credit na baadae kukataa kulipa madeni yake na kisha kukimbilia mahakamani, huko walipewa ushindi.
DELINA GROUP (mali ya Davis Mosha), wamekopa CRDB BANK TZS 4 bilioni na KCB BANK $15 milioni ambapo mkopaji alikimbilia mahakamani na kesi yake kuendeshwa na jaji wa ile kesi ya TSN GROUP.
BIGBON PETROLEUM CO. LTD. Walikopa TZS 22 bilioni NBC BANK wakagoma kulipa. Ni nyakati hizo, baadhi ya mali za kampuni hiyo (nyumba zilizokuwa dhamana) katika maeneo ya Kariakoo ziliwaka moto
Masasi Construction Co. Ltd, B.H.Ladwa Ltd, ZAS Investment Company; Kampuni zinamilikiwa na mtu mmoja wamekopa TZS 22 bilioni EQUITY BANK na kukataa kulipa mkopo kwa kukimbilia mahakamani.
ZAS Investment Co. LTD inadaiwa na EQUITY BANK Tanzania LTD TZS 22 bilioni, zikiwa ni mkopo ambao iliiipatia kampuni hiyo kwa ujenzi wa hoteli kwa nyakati tofauti kuanzia 2017, pamoja na riba.
Mahakama Kuu kanda ya DSM, ilitupilia maombi ya ZAS Investment Co. LTD kutaka kuhamisha kesi kutoka kwa Jaji Edwin Kakolaki kwenda kwa Jaji Butamo Phillip. Wakili wa ZAS ni Frank Mwalongo.
GLOBAL AGENCY Co. LTD (Mali ya Fidelis Bashasha); imekopa kiasi cha TZS 26 bilioni benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) na kukopa pia bilioni 14 EQUITY BANK na kote huko imekataa kulipa madeni yake.
STATE OIL (T) Ltd (Nilesh Suchak); wamekopa TZS 7 bilioni CRDB, wakakopa TZS 4 bilioni ABC BANK, wakakopa $26 milioni EQUITY BANK na kukataa kulipa. Wakakimbilia mahakamani. Kesi wameshinda
Continental Reliable Clearing (T) Limited (CRC); (mali ya Abri family Iringa), wamekopa na kukataa kulipa $2 milioni, STANBIC BANK. Pia EXIM BANK $3 milioni na EQUITY BANK $11 milioni (zaidi ya TZS 30 bilioni)
Continental Reliable Clearing (T) Limited (CRC) iko hatarini kufungwa kutokana na shauri lililofunguliwa na EQUITY BANK, Equity Bank (T) LTD na Equity Bank (K) LTD, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Benki hizo zinaidai Continental Reliable Clearing (T) Limited (CRC) zaidi ya $10.5 milioni na TZS 780.6 milioni. Shauri hilo lipo chini ya Jaji Butemo Phillip. CRC wanawakilishwa na Wakili Frank Mwalongo.
Kwa mujibu wa Wakili wa EQUITY, Shalom Samuel Masakyi, CRC imekimbilia mahakamani kujaribu kuzuia uuzwaji wa dhamana ilizoweka kuchelewesha kulipa madeni ili dhamana hizo zisiuzwe.
Nas Hauliers Ltd; walikopa na kukataa kulipa kiasi cha $16 milioni za EQUITY BANK. Wakakimbilia mahakamani. Nas Hauliers Ltd wakapewa ushindi mahakamani dhidi ya EQUITY BANK (T) Ltd.
Jaji Deo John Nangela aliandika hukumu ndefu ya kurasa 164 19/04/2023 akiwapa ushindi Nas Hauliers Ltd katika COMMERCIAL CASE NO. 105 OF 2021 katika High Court Commercial Division
Nini tafsiri ya mambo yote niliyoelesa hapo juu? Ni kwamba fedha za mitaji ya watu wa hali ya chini zinatumika kunufaisha watu wachache wanaojua kuichezea mahakama. Mahakam ipo mfukoni.
Kwa kesi tajwa tu hapo juu zaidi ya TZS 800 bilioni zimeliwa na watu chini ya 10, kiasi ambacho wangekopeshwa wajasiriamali baada ya mikopo kurejeshwa maelfu ya vijana wangepata mikopo
Pesa za TADB ni pesa za serikali, kuzitafuna kihuni ni kutafuna pesa za umma na huo ni ufisadi kama ufisadi mwingine wowote ule. CAG sijaona akiangazia jambo hilo kabisa katika taarifa yake ya udhibiti na ukaguzi.
Pesa za NBC, CRDB, NMB ni pesa mchanganyiko wa watu binafsi na pesa za serikali hivyo kuzitafuna pesa hizo ni kutafuna pesa za umma. Serikali imeweka pesa za umma katika benki hizo tajwa hapo juu.
Zaidi ya asilimia 95 ya benki ya AZANIA ni mifuko ya hifadhi za jamii hasa NSSF, hivyo kuchukua pesa AZANIA BANK bila kurudisha ni sawa na kutafuna vikokotoo vya wastaafu wa serikali na sekta binafsi
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni 3nd largest shareholder wa AZANIA Bank (17.97%) na walichukua pesa za wanachama zaidi ya Sh200 bilioni kununua hisa Azania Bank ambayo haijawahi KUTOA GAWIO
Kwa ujumla mahakama inapaswa ijitathmini upya. Mfumo wa mahakama umeoza, umesheheni rushwa na unapaswa kurekebishwa upya. Kama mahakama zinachezewa hivi, nchi yetu haipo salama kabisa.
Heshima na hadhi ya mahakama inalindwa kwa matendo ya watendaji wa mahakama. Ukirejea hizi kesi, zinachafua hadhi, sifa na taswira ya mahakama. Korido za mahakama zimekuwa vyumba vya rushwa?
BoT lazima wasimame kupitia vitengo vyake kuhakikisha inalinda mitaji ya benki hizi, benki zote mitaji yake ni fedha kidogo kidogo zinazowekwa kama akiba za wananchi mbalimbali ikiwemo maskini.
Kituo cha uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre TIC) watazame upya namna gani wanalinda uwekezaji. Hapa kuna benki za nje na ndani ya nchi (EQUITY na KCB ni benki za nje), zimetapeliwa.
Kuwaruhusu hawa wafanyabiashara kutapeli mabilioni ya pesa kutumia mahakama za ndani ni sawa na kufedhehesha sera za uwekezaji ambazo serikali inazunguka huko Duniani kuzitangaza.
JAJI MKUU lazima achukue hatua haraka kusafisha taswira na kulinda hadhi ya mahakama ya Tanzania. Jaji Mkuu ndiye tumemkabidhi mahakama zetu, azisimamie zikitemda haki kwa makundi ya aina zote.
Tuhuma za majaji kulambishwa asali zimekuwa nyingi, tuhuma za majaji kupewa maelekezo na wanasiasa ili kutoa upendeleo zimekuwa zikiongezeka kila siku. Je, JAJI MKUU umeridhika?
Mwisho, kwa kuwa kidole hiki naelekeza katika mhimili muhimu wa kutafsiri sheria na kutoa haki, hivyo, katika hili ni muhimu sana JAJI MKUU mapema utazame wapi panapovuja ukazibe.
Nakala kwa; Rais @SuluhuSamia @ikulumawasliano @mwigulunchemba1 @judiciarytz @InvestTanzania
Martin Maranja Masese, MMM.
Juzi gazeti hili lilipoti kuwa
Jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukaribisha na kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchini unaelezwa kutiwa kigingi na tabia chafu inayozidi kuota mizizi ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kushirikiana na baadhi ya majaji wa mahakama kuu wasio waaminifu kuyatapeli mabenki ya ndani na nje ya nchi kwa na hivyo kuwanyima fursa wafanyabiashara wadogo na wakati kushindwa kuaminiwa na kupata mikopo.
Orodha ya wafanyabiashara wanaotumia mahakama kutapeli na kudhulumu mabenki iliyofanyiwa uchunguzi na kuthibitishwa na gazeti hili, inaonyesha kuwa wengi kati ya wafanyabiashara hao wanajihusisha na biashara za Mafuta na ushafirishaji ambapo wastani wa shilingi za kitanzania Trilioni 1.3 wamekopa katika benki mbalimbali za ndani nan je ya nchi na kukataa kulipa kisha kukimbilia mahakamani ambako pia wanadaiwa kupata ushindi kwa njia zisizo za kawaida
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wafanyabiashara hao wanaoheshimika nchini wakionekana machoni mwa watu kuwa ni matajiri na wengine wakijionyesha kama wacha Mungu na wenye kumuogopa Mungu huku wengine wakijinasibu kama wana michezo na wawekezaji wakubwa wanaitumia mahakama hasa mahakama ya biashara kama kichaka chao cha kufanyia uhalifu huo wa kimkakati
‘’hebu fikiria, mtu amekwenda TADP amekopa bilioni 40, akaenda Azania benki akakopa bilioni 70, hajaishia hapo akaenda Equity benki akakopa bilioni 110, halafu akapanda ndege hadi ujerumani akavidanganya baadhi ya viwanda vya huko kuwa anaenda kuwekeza mafuta Kahama, nako wakamkopesha mali na mtaji wa zaidi ya bilioni 220, halafu anakataa kulipa mkopo makusudi kwa kukimbilia Mahakamani na Jaji anampa ushindi bila kuzingatia Ushahidi na ukweli kuwa hizo bilioni 220 za ndani na bilioni 220 alizochukua ujerumani zote kwa pamoja zinaingia kwenye deni la Taifa na kukataa kwake kulipa mkopo kunatunyima fursa sisi wafanyabiashara wadogo kuaminiwa’’. Anasema Christopher Kabison mfanyabiashara wa vifaa vya simu Kariakoo
Kabison anaongeza kuwa kama Serikali haitachukua hatua za haraka kuingilia kati hali hii basi jitihada za Rais kutaka mabenki yakopeshe wafanyabiashara kwa riba nafuu zitabaki kuwa ndoto kwani hakuna benki itakayokuwa tayari kuendelea kupoteza mitaji yake huku mahakama zinazotarajiwa kuwa ni sehemu ya haki zikitumika kuhalalisha uchafu huo
‘’juzi nilikuwa napitia hukumu za mahakama, nimeshuhudia jaji mmoja amempa ushindi Stati oili ambaye alikopa dola milioini 26 equiti benki halafu akakataa kulipa, ukizipitia hizi hukumu unaweza ukajiuliza kama jaji wakati anatoa hukumu alikuwa sawa sawa ama ameonja kidogo..na jaji huyo huyo akahukumu hukumu kama hiyo kwa kampuni ya derina ambayo ilikopa zaidi ya bilioni 40 na kukataa kulipa. Sasa hapa tukisema mahakama inatumika kuhalalisha ujambazi dhidi ya watanzania tutakuwa tumeionea’’. Aliongeza Kobisoni
Kwa mujibu wa taarifa na nyaraka ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa miongoni mwa makampuni yanayoongoza kufilisi mabenki huku wakitumia mahaka ni pamoja na KOM GROUP ambayo imeweka kibindoni zaidi ya bilioni 440 na kukataa kulipa na kuziacha solemba benki za TADB,AZANIA pamoja na EQUITY sambamba na ujerumani
Wengine wanaoongoza genge la kukwamisha jitihada za Rais Dkt. Samia katika kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kukataa kulipa mikopo na kisha kukimbilia mahakamani na mahakama kuwapa hukumu za ushindi ni pamoja na kampuni ya TSN iliyozidhulumu benki za NMB na Equity, Derina Group iliyozidhulumu benki za CRDB na KCB huku BIG BON ikitajwa kuidhulumu benki ya NBC kama ambavyo Masasi construction inavyopambana kuidhulumu benki ya Equity kwa kutumia mahakama
Sambamba na kampuni hizo, nyingine ni Global Agency, State Oil inayomilikwa na Nilesh Suchak kama ilivyo kwa NAS HAULIERS na Continental reliable zinazotamba kuwadhulumu CRDB, NMB, NBC,EQUITY, KCB na nyinginezo
Ikiwa kitendo hiki cha wafanyabiashara hawa wakubwa kukopa na kuacha kulipa madeni kisha kukimbilia mahakamani na mahakama kuwapa ushindi kitaachwa kuendelee kuota mizizi kitapelekea Taifa kuwa na kikundi ‘GANG’ cha wafanyabiashara wanaoutawala Uchumi wa nchi na hivyo kuhatarisha amani ya Taifa
Kuwepo nje ya mzunguko wa benki hizi mabilioni hayo ya shilingi ni kiashiria kibaya katika ukuzaji wa Uchumi huku Gavana wa benki kuu akiombwa kuchukua hatua za haraka kuingilia sintofahamu hii inayozidi kushika kasi
‘’kama BOT hawatakuwa serious na kuingilia kati kunusuru hili jambo, benki zitafungwa hizi, ama zisipofungwa basi Uchumi utahama kutoka kuwa rasmi na kuwa Uchumi wa kihuni unaondeshwa na wahuni, lazima benki kuu iingilie kati haraka’’. Alisema Juma Hamad mchambuzi wa masuala ya kiuchumi
Aliongeza kuwa katika Taifa lolote ambalo linaheshimu utawala wa sheria, ni nadra kwa wafanyabiashara kukopa halafu kukataa kulipa makusudi kisa tu kuna mahakama, hali hii inaweza kushawishi na wafanyabiashara wadogo nao kukataa kulipa na ikiwa wakashindwa mahakamani basi itasababisha hali ya sintofahamu
Gazeti hili linaendelea na jitihada za kuwatafuta wote waliotajwa kukapua mabilioni hayo na kukataa kulipa huku simu zao za mkononi zikiita bila kupokelewa.
Gazeti hili litaendelea kuweka wazi mchezo wote