- Wafanyabiashara wakubwa wadaiwa kudhulumu mabenki kutumia mahakama
- Wachota mabilioni ya akiba za wateja na kujinufaisha, wagoma kulipa wkimbilia mahakamani mahakama yabariki
- Mmoja akwapua bilioni 40 TADB, akakwapua bilioni 70 Azania, akakwapua bilioni 110 Equity kisha akapiga bilioni 220 ujerumani
- Mwengine kachukua bilioni 15 NMB, akachukua bilioni 80 EQUITY akagoma kulipa akakimbilia mahakamani Jaji akampa ushindi anaendelea kutanua mitaani
- Jaji huyo huyo na kwa staili hiyo hiyo akampa ushindi mfanyabiashara mwingine aliyekwapua dola milioni 15 KCB
- Jitihada za Rais Dkt. Samia kuvutia uwekezaji zinazidi kukwamishwa, BOT, TIC, watakiwa kujipanga upya
Na. Mwandishi wetu,
Jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukaribisha na kuhamasisha uwekezaji wa ndani na kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchini unaelezwa kutiwa kigingi na tabia chafu inayozidi kuota mizizi ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kushirikiana na baadhi ya majaji wa mahakama kuu wasio waaminifu kuyatapeli mabenki ya ndani na nje ya nchi kwa na hivyo kuwanyima fursa wafanyabiashara wadogo na wakati kushindwa kuaminiwa na kupata mikopo.
Orodha ya wafanyabiashara wanaotumia mahakama kutapeli na kudhulumu mabenki iliyofanyiwa uchunguzi na kuthibitishwa na gazeti hili, inaonyesha kuwa wengi kati ya wafanyabiashara hao wanajihusisha na biashara za Mafuta na ushafirishaji ambapo wastani wa shilingi za kitanzania Trilioni 1.3 wamekopa katika benki mbalimbali za ndani nan je ya nchi na kukataa kulipa kisha kukimbilia mahakamani ambako pia wanadaiwa kupata ushindi kwa njia zisizo za kawaida
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wafanyabiashara hao wanaoheshimika nchini wakionekana machoni mwa watu kuwa ni matajiri na wengine wakijionyesha kama wacha Mungu na wenye kumuogopa Mungu huku wengine wakijinasibu kama wana michezo na wawekezaji wakubwa wanaitumia mahakama hasa mahakama ya biashara kama kichaka chao cha kufanyia uhalifu huo wa kimkakati
‘’hebu fikiria, mtu amekwenda TADB amekopa bilioni 40, akaenda Azania benki akakopa bilioni 70, hajaishia hapo akaenda Equity benki akakopa bilioni 110, halafu akapanda ndege hadi ujerumani akavidanganya baadhi ya viwanda vya huko kuwa anaenda kuwekeza mafuta Kahama, nako wakamkopesha mali na mtaji wa zaidi ya bilioni 220, halafu anakataa kulipa mkopo makusudi kwa kukimbilia Mahakamani na Jaji anampa ushindi bila kuzingatia Ushahidi na ukweli kuwa hizo bilioni 220 za ndani na bilioni 220 alizochukua ujerumani zote kwa pamoja zinaingia kwenye deni la Taifa na kukataa kwake kulipa mkopo kunatunyima fursa sisi wafanyabiashara wadogo kuaminiwa’’. Anasema Christopher Kabison mfanyabiashara wa vifaa vya simu Kariakoo
Kabison anaongeza kuwa kama Serikali haitachukua hatua za haraka kuingilia kati hali hii basi jitihada za Rais kutaka mabenki yakopeshe wafanyabiashara kwa riba nafuu zitabaki kuwa ndoto kwani hakuna benki itakayokuwa tayari kuendelea kupoteza mitaji yake huku mahakama zinazotarajiwa kuwa ni sehemu ya haki zikitumika kuhalalisha uchafu huo
‘’juzi nilikuwa napitia hukumu za mahakama, nimeshuhudia jaji mmoja amempa ushindi Stati oili ambaye alikopa dola milioini 26 equiti benki halafu akakataa kulipa, ukizipitia hizi hukumu unaweza ukajiuliza kama jaji wakati anatoa hukumu alikuwa sawa sawa ama ameonja kidogo..na jaji huyo huyo akahukumu hukumu kama hiyo kwa kampuni ya derina ambayo ilikopa zaidi ya bilioni 40 na kukataa kulipa benki ya KCB. Sasa hapa tukisema mahakama inatumika kuhalalisha ujambazi dhidi ya watanzania tutakuwa tumeionea’’. Aliongeza Kobisoni
Kwa mujibu wa taarifa na nyaraka ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa miongoni mwa makampuni yanayoongoza kufilisi mabenki huku wakitumia mahaka ni pamoja na KOM GROUP ambayo imeweka kibindoni zaidi ya bilioni 440 na kukataa kulipa na kuziacha solemba benki za TADB,AZANIA pamoja na EQUITY sambamba na ujerumani
Wengine wanaoongoza genge la kukwamisha jitihada za Rais Dkt. Samia katika kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kukataa kulipa mikopo na kisha kukimbilia mahakamani na mahakama kuwapa hukumu za ushindi ni pamoja na kampuni ya TSN iliyozidhulumu benki za NMB na Equity, Derina Group iliyozidhulumu benki za CRDB na KCB huku BIG BON ikitajwa kuidhulumu benki ya NBC kama ambavyo Masasi construction inavyopambana kuidhulumu benki ya Equity kwa kutumia mahakama
Sambamba na kampuni hizo, nyingine ni Global Agency, State Oil inayomilikwa na Nilesh Suchak kama ilivyo kwa NAS HAULIERS na Continental reliable zinazotamba kuwadhulumu CRDB, NMB, NBC,EQUITY, KCB na nyinginezo
Ikiwa kitendo hiki cha wafanyabiashara hawa wakubwa kukopa na kuacha kulipa madeni kisha kukimbilia mahakamani na mahakama kuwapa ushindi kitaachwa kuendelee kuota mizizi kitapelekea Taifa kuwa na kikundi ‘GANG’ cha wafanyabiashara wanaoutawala Uchumi wa nchi na hivyo kuhatarisha amani ya Taifa
Kuwepo nje ya mzunguko wa benki hizi mabilioni hayo ya shilingi ni kiashiria kibaya katika ukuzaji wa Uchumi huku Gavana wa benki kuu akiombwa kuchukua hatua za haraka kuingilia sintofahamu hii inayozidi kushika kasi
‘’kama BOT hawatakuwa serious na kuingilia kati kunusuru hili jambo, benki zitafungwa hizi, ama zisipofungwa basi Uchumi utahama kutoka kuwa rasmi na kuwa Uchumi wa kihuni unaondeshwa na wahuni, lazima benki kuu iingilie kati haraka’’. Alisema Juma Hamad mchambuzi wa masuala ya kiuchumi
Aliongeza kuwa katika Taifa lolote ambalo linaheshimu utawala wa sheria, ni nadra kwa wafanyabiashara kukopa halafu kukataa kulipa makusudi kisa tu kuna mahakama, hali hii inaweza kushawishi na wafanyabiashara wadogo nao kukataa kulipa na ikiwa wakashindwa mahakamani basi itasababisha hali ya sintofahamu
Gazeti hili linaendelea na jitihada za kuwatafuta wote waliotajwa kukapua mabilioni hayo na kukataa kulipa huku simu zao za mkononi zikiita bila kupokelewa.
Gazeti hili litaendelea kuweka wazi mchezo wote