Na.Stanslaus Kivumbi, Tanga
Miradi ya maji katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga yenye wastani wa thamani ya shilingi bilioni 10 iliyo katika hatua mbalimbali za utekeelzaji chini ya wakala wa usambazaji maji vijijini Ruwasa inatarajia kuangazwa na mbio za mwenge wa uhuru mkoani Tanga mwaka huu, mbio zinazokimbizwa na Godfrey Eliakim Mzava
Miongoni mwa miradi hiyo inayotarajia kuwadumia maelfu ya wakazi wa mkoa huo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa maji kwakibuyu kata ya kipumbwi wilayani pangani wenye thamani ya shilingi milioni 594 ambapo uzinduzi wa ujenzi wa mradi utafanyika,
Kata ya Kwamsisi wilayani Handeni panatarajiwa pia kuwepo kwa uzinduzi wa mradi katika mradi wa ujenzi wa mradi wa maji kwamzara wenye thamani ya milioni 132 za kitanzania,
Kadhalika wilayani korogwe mwenge utaangazia kata ya Magila gereza kwenye mradi wa maji wa Magira Gereza wenye thamani ya shilingi milioni 765 na kuweka jiwe la msingi kuashiria ujenzi wa mradi huo kuanza
Miradi mingine inayotarajiwa kukaguliwa, kuzinduliwa ama uwekaji wa jiwe la msingi ni pamoja na mradi kata ya Lushoto wenye thamani ya billion 1 na milioni 800, mtadi wa kata ya funta iliyopo bumbuli wenye thamani ya shilingi milioni 823, mradi wa mapatano wilayani mkinga wenye thamani ya shilingi bilioni 1 na milioni 500 sambamba na mradi wa Gombero ambapo ukarabati mkubwa utafanyika katika mradi huo ukitaraji kugharimu shilingi bilioni 3 na milioni 150 huku madi wa bokwa wilayani kilindi unaogharimu shilingi milioni 765 ukiwekewa jiwe la msingi pia
Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 una kaulimbiu “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelezu”