Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewasili Wilayani Mpanda, Mkoani Katavi katika ziara yake ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, leo tarehe 08 Aprili 2024.
Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua utekelezaji wa miundombinu ya barabara ikiwemo ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Sitalike – Kibaoni (km 70) iliyopo katika Halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi.