- Ni hifadhi iliyo rahisi kufikika kwa gari kupitia barabara ya Tanzania-Zambia ambapo unaweza panda gari ukashushwa getini
- Ni hifadhi inayozungukwa na mikoa ya kibiashara na kimkakati ya Morogoro, Dar, Dodoma na Iringa
- Vyumba vya kulala hifadhini bei chee ambapo vinaanzia shilingi elfu tano hadi elfu 23
- Gharama ya chakula na vinywaji hifadhini ni nafuu sana ambapo mgeni anaweza kula hata chakula cha shilingi 1500
- Zinatua ndege moja kwa moja kutoka Zanzibar
- Jina la MIKUMI linatokana na mti maarufu wa mkoche ambao kwa lugha ya wenyeji wanauita MKUMI
- Ni familia moja tu ndio inayoweza kuingia katika bwawa la viboko na mamba kufanya usafi wa bwawa hilo huku wanyama hao wakiwemo ndani
Na Mwandishi Wetu , MOROGORO
HIFADHI ya Mikumi imesema kuwa watanzania kutalii hifadhi pamoja na kupata malazi katika hifadhi hiyo ni gharama shilingi 23000.
Hayo ameyasema Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Agustine Masesa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo.
Watanzania wamekuwa wakifikifiria kufanya utalii katika hifadhi hiyo ni gharama kubwa ambapo Hifadhi hiyo imeweka mazingira rafiki ya kila mtanzania kufanya utalii katika hifadhi ya Mikumi kutokana na kuwa na miundombinu rafiki ikiwemo Barabara ya lami pamoja na Reli pamoja na Ndege
Masesa amesema Hifadhi ya Mikumi ndio hifadhi inayoongoza kwa idadi kubwa ya watalii wa ndani kutokana na Jiographia yake ya Kufikika kwa urahisi.
Amesema kuwa katika hifadhi ya Mikumi kwa mtalii wa ndani kupata huduma ya chakula ndani ya hifadhi kwa sh.2000 lengo ni kila mtanzania kufanya utalii katika hifadhi hiyo kiwango kidogo cha kiingilio cha 5000.
Mkuu wa Uhifadhi Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Masesa Amesema kuwa wamejipanga kuona watanzania wanavutika kutembelea hifadhi hiyo na kuona vivutio vingi ambavyo adimu katika hifadhi hiyo.
Hata hivyo amesema wanyama wanaopatikana katika hifadhi hiyo ni Simba ,Tembo, Chui ,Faru pamoja na Tembo huku kukiwa na wanyama wengine wengi ukiachana wanyama wa Big Five
Amesema kuwa wakati umefika kwa kika mtanzania kuwa katika mipango yao ni pamoja na kufanya utalii katika hifadhi ya Mikumi.
Amesema kuwa unaweza kutalii hata kwa magari binafsi katika hifadhi hiyo bila kutumia magari ya kukodi kutembezwa.
Masesa amesema watanzania waunge jutihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika filamu ya Royal Toure nao kutembelea hifadhi ya Mikumi.
Amesema Hifadhi hiyo ina vivutio vya aina yake ambayo huwezi kuona katika hifadhi nyingine hivyo watanzania wakitaka kujua asili yao kutembelea Mikumi.