Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Nigeria, Michael Adebayo Olayinka, anayejulikana sana kama Ruger, amezindua studio yake mwenyewe inayoitwa ‘Blown Boy Ent.’
Tangazo hilo lilitolewa kupitia Instagram story ya Ruger mnamo Ijumaa, Januari 19, 2024.
Katika video fupi iliyoonyesha msanii huyo akiweka lebo yake mpya ya kurekodi, @blownboyent, kuashiria kukaribia kutolewa kwa wimbo mpya chini ya bango la Blown Boy.
Wasifu wa hitmaker huyo kwenye Instagram pia umesasishwa ili kuonyesha jina la label hiyo.
Wakati Ruger hajaeleza rasmi kuachana na lebo yake ya awali, Jonzing World, hatua hiyo imezua msisimko miongoni mwa mashabiki, wanaotamani matoleo yajayo ya msanii huyo na kutarajia safari ya kipekee ya kimuziki atakayoianza akiwa na Blown Boy Ent.