CHADEMA SIKIO LA KUFA
NA MWANDISHI WETU
MTIFUANO mpya umeibuka ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar, Said Issa Mohammed na wenzake watatu, kufungua kesi Mahakama Kuu wakitaka kisimamishwe kwa muda kujihusisha na shughuli zote za kisiasa nchini.











