Zari: Sina uhusiano na Diamond

0

Na Mwandishi Wetu

Mfanyabaishara Zarina Hassan maarufu Zari The Bosslady amesema kinachoendelea katika yake na mzazi mwenzake, msanii Diamond Platnumz ni ushiriki wa majukumu ya wazazi kulea watoto wao tu.

Zari hayo ameeleza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kauli ya Zari inakuja wakati kukiwa na tetesi zinazodai kuwa wawili hao wamerudiana mara baada ya kuachana toka mwaka 2018 na kila mmoja kuwa na maisha yake.

Alhamis Novemba 5, 2020 wikiiliyoisha, Zari akiwa ameongozana na watoto wake wawili, Tiffah na Nillan walikuja Tanzania wakitokea Afrika Kusini wanapoishi, Zari alieleza kuwa ameleta watoto kuonana na Baba yao.

Tangu Zari katua nchini amekuwa akionekana na Diamond kwenye matukio mbalimbali pamoja na familia ya msanii huyo kitu kinachoibua hisia kuwa wawili hao wamerudiana.

Zari aliweza kutembelea Wasafi Media inayomilikiwa na Diamond kwa mara ya kwanza, pia waliongozana hadi kiwanda cha kutengeneza vinywaji baridi vya Pepsi ambapo Diamond ni balozi, kubwa zaidi ni pale walipoenda wote kutazama mchezo kati ya Simba na Yanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here