Zanzibar: Majina ya wapiga kura yawekwa wazi

0

Na Mwandishi Wetu

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imeweka wazi daftari la kudumu la wapigakura kwa kubandika daftari hilo katika kila kituo cha kupigia kura Unguja na Pemba.

Mkurugenzi ZEC, Thabit Idarous Faina akizungumza na waandishi wa hahari leo Jumatano Oktoba 21 wakati wa ubandikaji wa daftari hilo, Rahaleo mjini Ungujaa amesema taftari hilo limebadikwa kwa ajili ya wapigakura kuangalia majina yao pamoja na vituo vya kupigia kura.

Amesema kazi ya uwekaji wazi daftari la wapigakura inafanyika kwa mujibu wa sheria.

Faina  amesema katika daftari hilo, jumla ya wapigakura 566, 352 wamesajiliwa kwa ajili ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Amesema kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria Tume inatakiwa kuweka wazi daftari la wapigia kura babla ya siku saba ya kufanyika uchaguzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here