Yanga yaondoa ukame wa magoli, yaichapa Mwadui 5-0

0

NA JONAS MUSHI

TIMU ya wananchi Yanga SC imeondoa ile njaa ya muda mrefu ya magoli jangwani baada ya kuichapa klabu ya Mwadui goli 5-0 katika uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Yanga imeshinda jana ikiwa ni mchezo wake wa 15 na kujichukulia alama tatu zinazoifanya kujikita zaidi keleleni ikiwa na jumla ya alama 37 mbele ya Azam FC yenye alama 27 ikifuatiwa na Simba nafasi ya tatu na alama 26 zikiwa zimecheza michezo 14.

Bao la dakika ya 6 la Deus Kaseke lilianzisha safari ya magoli mengine manne ya Yanga  katika mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wengi. Kaseke alifunga goli zuri baada ya kupokea pasi kutoka kwa mshambuliaji mwenzake Mukoko.

Mchezo uliendelea Yanga wakitawala zaidi kwa kupiga pasi nyingi na kutengeneza nafasi za mashambulizi dhidi ya Mwadui na dakika ya 14 mshambulia Yacouba Sogne aliandika bao la pili kwa Yanga naye akipokea pasi kutoka kwa Mukoko kasha kuutuliza mbele ya beki wa Mwadui kisha kumzuka na kuachia shuti kali lililoenda upande wa kulia na kumwacha chini goli kipa.

Timu zilienda mapumziko Yanga ikiwa bele kwa goli 2-0 na zilirejea uwanjani kukiwa hakuna mabadiliko ya mchezaji yeyote.

Dakika ya 49 Yacouba aliiandikia timu yake goli la tatu na kuzidi kupoteza matumaini ya Mwadui katika mchezo huo ikiwa nyumbani kwake.

Mwadui ikiwa imeelemewa hasa katika nafasi ya katikati huku ikishindwa kupeleka mashambulizi katika lango la Yanga iliipa Yanga nafasi ya kutamba katika eneo lao la hatari na kufikia dakika ya 56 TK Master Tuisila Kisinda aliandika bao la nne kwa mkwaju mkali mbele ya mabeki wa Mwadui.

Dakika ya 60 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Deus Kaseke na kumwingiza Haruna Niyonzima ambaye alionyesha ufundi wake wa kupiga pasi zilizokuwa zinafika sawasawa na kuongeza kasi ya mashambulizi.

Dakika ya 67 Yanga ilifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Yacouba na kumwingiza Farid Mussa ambaye aliongoza mashambulizi kutoka pembeni upande wa kushoto.

Mabadiliko hayo yalizaa matunda dakika ya 70 ambapo bao la kapteni Lamine Moro ilikamilisha safu ya magoli yaliyoiandikia rekodi mpya Yanga kwa kupata magoli mengi katika mechi moja tangu kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mechi hiyo ya kusisimua ilimalizika dakika 90 Yanga ikiwa  kifua mbele na kujihakikishia kuendelea kukaa kileleni.

Kwingineko katika Ligi hiyo jana bao pekee la kiungo Salum Kihimbwa lilitosha kuipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 15 na kupanda nafasi ya tisa kutoka ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakati KMC inayobaki na pointi zake 21za mechi 13 sasa inabaki nafasi ya tano.

Dodoma Jiji nayo iliizamisha meli ya Gwambina FC kwa ushindi mwembamba wa goli moja kwa sufuri mchezo uliopigwa kunako dimba la Jamhuri jijini Dodoma

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here