Yanga, Tanzania Prisons nani mbabe

0

NA MWANDISHI WETU, SUMBAWANGA

WAKATI Ligi Kuu ikiendelea leo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ametoa tahadhari kwa timu za Yanga na Tanzania Prison kutoingia uwanjani na matokeo katika mchezo wao wa mzunguuko wa pili utakaochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Ikumbukwe timu hizo mbili zilipokutana katika mzunguuko wa kwanza jiji Dar es Salaam hakukuwa na mbabe aliyeweza kuondoka na alama zote tatu.

Kutokana na mazingira hayo, yanafanya vinara wa ligi hiyo kukamia kupata pointi tatu ugenini huku Tanzania Prison ikikataa kuwa mnyonge katika uwanja wa nyumbani na hivyo kutokubali kufungwa na kuwakumbusha kuwa mchezo una matokeo matatu na kila timu iwe tayari kuyapokea matokeo hayo.

“Wapenzi wa mpira wa miguu wafike kwa wingi waweze kujione mshindi atakuwa ni nani, kwasababu mpira una matokeo matatu, kuna kushinda, kufungwa lakini pia kuna sare.

“Timu zote mbili zijiandae kwa matokeo hayo matatu, isije mtu anakuja na matokeo yake hapa kwamba mimi nitashinda halafu akashindwa halafu akafanya fujo.

“Sisi vyombo vya ulinzi na usalama tumeshajiweka vizuri kwa fujo zozote ambazo mtu amejiandaa nazo aziache huko huko,”alisisitiza.

Wangabo , aliyasema hayo alipokwenda kuutembelea Uwanja wa Nelson Mandela ili kujionea maandalizi ya uwanja huo kabla ya mechi ya ligi kuu baina ya timu hizo itakayochezwa katika uwanja huo kabla ya mkesha wa mwaka mpya wa 2021.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, aliapa kuanza kwa kishindo mzunguko wa pili kwa kuondoka na ushindi dhidi wajelajela ha leo.

Kaze ambaye alikiongoza kikosi hicho hadi sasa kikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, alisema anazitaka pointi tatu katika mchezo huo ili kuzidi kuyakaribia malengo yao.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli, alisema wakati wakiendelea na maandalizi ya mchezo huo wakiwa jijini Mbeya, Kocha Kaze alikuwa akisisitiza kwamba lazima wauanze mzunguko wa pili na pointi tatu za Prisons.

“Tumejiandaa vema na mechi za mzunguko wa pili chini ya Kocha Kaze ambaye aliwapa mapumziko mafupi wachezaji na sasa tumeingia vitani kwa kufanya mazoezi baada ya sikukuu.

“Tunafahamu wapinzani wetu Prisons wapo nyumbani, lakini sisi hatujali, tutapambana kuhakikisha tunafanikiwa kupata ushindi mnono leo,”alisema Bumbuli

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here