Yajue majengo marefu zaidi Barani Afrika

0

  >>Limo pia jengo la Bandari na PSPF 

NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM

HISTORIA  ya majengo marefu zaidi barani Afrika ilianza mwaka 1973 kufuatia ujenzi wa jumba refu la Carlton Centers mjini Johannesburg , ambalo lilishikilia taji la jumba refu barani Afrika hadi mwezi Aprili 2019 kulingana na mtandao wa CK .

Baada ya kupata sifa ya kuwa na jumba refu zaidi barani , haishangazi kuona kwamba Afrika Kusini imejizatiti kumiliki idadi kubwa ya majumba marefu barani Afrika.

Majumba hayo si tu yanapendezesha miji husika bari pia ni kichocheo cha uchumi kwakuwa ndani ya majengo kunakuwa na ofisi nyingi ambazo zinamsaidia mtu ama taasisi husika kuingiza fedha na kukuza uchumi.

Jengo la kwanza ni  Leonardo, Afrika Kusini,jumba la Leonardo lina urefu wa mita 227-pamoja na ghorofa 56. Jumba hilo lilipo katika barabara ya 75 ya Maude, takriban mita 100 kutoka katka jumba la hisa la Johannesburg Stock Exchange.

Kulingana na mtandao wa CK, ujenzi wa jumba hilo ulianza tarehe 17 mwezi Novemba 2015 na liliongoza mwaka 2019 , likishinda rasmi taji la kuwa jumba refu zaidi barani Afrika.

Jengo la pili ni  Carlton Centre, Afrika Kusini,Jumba la Carlton Centre, lenye urefu wa mita 223 ni kituo kikuu cha maduka tofauti – mjini Johannesburg, Africa kusini, limekuwa jumba refu barani Afrika kwa muda mrefu kabla ya ujenzi wa jumba a Leonardo 

Pia kuna jengo la Britam Tower la Kenya,Britam Tower, lina urefu wa mita 200 na limejengwa katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi . Lilifunguliwa ramsi kwa umma 2018 , na kulipiku jumba la UAP Old Mutual kama jumba refu zaidi nchini Kenya.

Jumba hilo lenye ghorofa 31 ambalo lilianza kujengwa mwaka 2013 lilikamilika mwezi Septemba 2017, na linajivunia muundo wa kipekee.

Mwaka 2018, Britam Tower lilikuwa jumba la kwanza barani Afrika kukabidhiwa taji la tuzo la Emporis Skyscraper lenye historia ya miaka 19 baada ya kutajwa kuwa jumba la kumi bora duniani.

Likiwa katika eneo la Upper hill jijini Nairobi jumba hilo lenye ghorofa 31 linatoa mandhari ya kupendeza ambapo unaweza kuona eneo la kati la mji mkuu wa Nairobi pamoja na maeneo ya viungani mwake ikiwemo mbuga ya wanyama pori ya Nairobi.

Ujenzi wake ulikamilika mnamo mwezi Novemba 2017, na sasa linamilikiwa na kampuni ya bima ya Britam Life Assurance Limited.

Katika siku nzuri isio na mawingu unaweza kuona Mt. Kilimanjaro pamoja na Mt Kenya juu ya jumba hilo.

Makao makuu ya CBE, Ethiopia,Jumba hilo lina urefu wa mita 198 na linamilikiwa na benki ya Commercial Bank ya Ethiopia (CBE) katikati ya mji mkuu wa Addis Ababa Ethiopia.

Ujenzi wake umemaliza utawala wa jumba la mikutano ya muungano wa Afrika AU mjini humo.

Jumba hilo lenye ghorofa 46 ambalo linaendelea kujengwa karibu na hoteli ya Ras Desta katika barabara ya Damtew litakuwa na mita 150,000 mraba likitarajiwa kuwa makao makuu ya benki hiyo inayomilikiwa na serikali.

Nairobi GTC Office Tower,ujenzi wa jumba la Nairobi GTC Office Tower, ambalo ndilo refu kati ya majumba sita ya Global Trade Centre, limeongeza mgeni mpya katika orodha ya majumba marefu nchni .

Juba hilo lenye urefu wa mita 184 na ghorofa 43 ndilo linalotarajiwa kuwa makao makuu ya kampuni ya China ya Avic ambayo inataka kujikita katika eneo la Westland mjini Nairobi.

Jumba hilo ambalo ujenzi wake ulianza Julai 2015 linatarajiwa kukamilika mwezi Disemba 2020.

Ponte City, Afrika Kusini,Jumba la Ponte City lenye urefu wa mita 172.8 lipo katika makaazi ya mji wa Johannesburg Afrika Kusini. Likiwa limejengwa 1975, jumba hilo lenye ghorofa 54 limetajwa kuwa jumba la kwanza la mviringo kujengwa Afrika

UAP Tower, Kenya,Jumba hili lililopo katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi lina urefu wa mita 163 . Liliwahi kuwa jumbe refu nchini Kenya na Afrika mashariki kwa jumla lilipofunguliwa mwezi Julai 2016 baada ya ujenzi wake uliochukua zaidi ya miaka mitano.

Awali Jumba la UAP Old Mutual jijini Nairobi ndio lililokuwa likishikilia nafasi ya jumba refu zaidi katika eneo la Afrika ya mashariki likiwa na ghorofa 33

Lilikuwa linafuatiwa katika orodha hiyo na Jumba la Twin Tower mjini Dar es salaam lenye ghorofa 35 na urefu wa mita 153.

NECOM House, Nigeria Kulingana na mtandao wa CK , Jumba la NECOM lililojulikana kama NITEL Tower na awali The NET Building, lina urefu wa mita 158 katikati ya mji wa Lagos .

Ndilo jumba refu lilio rasmi nchini Nigeria na eneo zima la Afrika magharibi. Jumba hilo lililokamilika 1979 ndio makao makuu ya kampuni ya Telecomunication Ltd iliokuwa ikimilikiwa na serikali.

Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA),Jumba la Tanzania Ports Authority Tower, lina urefu wa mita 157 katika mji wa kibiashara wa Dar esa Salaam.

Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA).

Baada ya ujenzi wake kukamilika 2016, jumba hilo lenye urefu wa mita 40 ndio makao makuu ya halmashauri ya Bandari nchini Tanzania.

Jengo la Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF)PSPF Towers, Tanzania,Jengo la PSPF Towers mjini Dar es Salaam nchini Tanzania lina urefu wa mita 153 na linatumika kama ofisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here