Wizara ya Kilimo yaagizwa kuratibu kilimo cha mazao ya bustani

0

Na Mwandishi Wetu 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameihakikishia taasisi ya Tanzania Horticulture Association (TAHA) kuwa shughuli zote kuendeleza kilimo cha bustani zitaratibiwa na Wizara ya Kilimo ili kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta hiyo.

Majaliwa amesema hayo leo (Jumamosi, Desemba 5, 2020) jijini Dar es Salaam alipokuwa anafungua kongamano la kikanda lililoangazia uwekezaji wa biashara ya mazao ya bustani.

“TAHA ni eneo moja kwenye maeneo yaliyopo katika kilimo hivyo, nataka niwahakikishieni matamanio yote mnayotaka kufikia katika kilimo cha bustani yatasimamiwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo,” amesema Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine, Majaliwa amesema kuwa serikali imejizatiti kuhakikisha shughuli za kilimo zinafanyika majira yote ya mwaka ili wakulima waweze kunufaika.

Akizungumza katika tukio hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na TAHA imefanya utafiti wa kina kuibua maeneo ya kufanyia kazi ili kuboresha miundombinu na mifumo ya maabara itakayosaidia kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo cha bustani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here