WHO yazindua kampeni ya ‘Jitolee kuacha kuvuta tumbaku’

0

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limezindua kampeni ya ‘Jitolee kuacha kuvuta’ kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutovuta Tumbaku kwa mwaka ujao wa 2021.

WHO imezindua kampeni hiyo katika mtandao wa WhatsApp, kwa kutoa chapisho liloliloandikwa “Zaidi ya sababu 100 za kuacha tumbaku” ikiwa ni kiashiria cha kuanza kwa kampeni hiyo.  

Taarifa ya WHO iliyotolewa hii leo mjini Geneva Uswisi imeeleza kuwa janga la COVID-19 limesababisha mamilioni ya watumiaji wa tumbaku kusema wanataka kuacha.

Kampeni hiyo itasaidia watu wasiopungua milioni 100 wanapojaribu kujitoa katika matumizi ya tumbaku.

‘Jitolee kuacha kuvuta’  itasaidia kuunda mazingira yenye afya ambayo yanafaa kuacha tumbaku kwa kutetea sera kali za kukomesha tumbaku, kuongeza

upatikanaji wa huduma za kukomesha, kuongeza uelewa juu ya mbinu za tasnia ya tumbaku na kuwawezesha watumiaji wa tumbaku kufanya majaribio ya kuacha yenye mafanikio

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here