WHO yatangaza idadi ya juu maambukizi corona

0

 NEWYORK, MAREKANI

SHIRIKA la Afya Duniani WHO, hapo jana limetangaza idadi mpya ya maambukizi ya virusi vya corona duniani kote ifikayo watu 581,679 ndani ya siku moja.

Zaidi ya watu milioni 48.5 wamethibitishwa kupata maambukizi hayo kote ulimwenguni, tangu janga la virusi vya corona kuanza mwanzoni mwa mwaka. Wataalamu wanatabiri idadi ya kweli ya maambukizi ni kubwa kuliko inayotangazwa rasmi.

Marekani, India na Brazil ndiyo mataifa yaliyoathirika zaidi kutokana na maambukizo hayo. Kulingana na takwimu za WHO, zaidi ya watu milioni 1.2 wamefariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19 unaotokana na virusi vya corona. Na jana pekee, zaidi ya vifo vya watu 8,900 vimethibitishwa katika saa 24.

Ujerumani imethibitisha maambukizi mapya zaidi ya 21,000 ndani ya siku moja,Huku nchi nyingine barani Ulaya zikizidisha hatua za kupambana na maambukizi. Huku nchi nyingine barani Ulaya zikizidisha hatua za kupambana na maambukizi.

Taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza nchini ya Robert Koch, imesema leo Ijumaa kwamba ya maambukizi imefikia 21,506 kwa muda wa saa 24, kutoka 19 elfu siku moja iliopita.

Hadi asubuhi ya jana, Ujerumani imethibitisha visa 619,000 tangu kuzuka kwa janga la virusi vya corona, huku watu 11,096 tayari wamekufa. Ingawa hali inayoendelea Ujerumani inaitia hofu serikali, mataifa mengine mengi ya barani Ulaya yanatajwa kuwa katika hali mbaya zaidi.

Maambukizi yaongezeka Ulaya

Uingereza imeanza kutekeleza hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona ikiwa ni pamoja na amri ya watu kubakia majumbani.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alitoa mwito wa pamoja kwa ajili ya kupambana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona. Huku Uingereza ikiweka amri ya watu kubakia nyumbani na kufungwa kwa biashara kwa kipindi cha wiki nne. Hatua sawa na hizo pia zinazingatiwa Uskochi, Wales, na Ireland ya Kaskazini.

Ufaransa, kuanzia jana imepiga marufuku migahawa na huduma ya chakula cha kuondoka nacho pamoja na kuuzwa kwa pombe kuanzia saa nne usiku hadi saa 12 asubuhi.

Nchini Italia, amri ya watu kutotoka nje usiku imeaanza kutekelezwa jana katika majimbo kadhaa. Hatua hiyo inatokana na tahadhari iliyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, kuhusu ongezeko la maambukizi barani Ulaya.

Rekodi mpya ya maambukizi Marekani

Marekani iliorodhesha idadi ya juu ya maambukizi ambayo ni zaidi ya 120,000 kwa muda wa saa 24, kwa mujibu wa hospitali ya Johns Hopkins. Marekani inaendelea kuongoza kwenye idadi ya watu waliokufa kutokana na corona ,ikiwa ni zaidi ya watu 234,000.

Kwingineko, Waziri Mkuu wa Sweden, Stefan Lofven, amejiweka karantini baada ya mtu wa karibu yake kuripotiwa kuwa na virusi vya corona. Ugiriki iliamuru watu kubaki nyumbani kwa kipindi cha wiki tatu, licha ya kwamba nchi hiyo ina idadi ndogo ya visa vya corona ukilinganisha na mataifa mengine ya Ulaya.

China inachukuwa hatua mpya dhidi ya wasafiri kutoka Ulaya. Brazil, ni nchi ya pili duniani baada ya Marekani ambayo imaethiriwa sana ikiwa na vifo zaidi ya 161,000. Ikifuatiawa na India ambayo tayari ina vifo zaidi ya 124,000.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here