Wema wamponza Mwanamuziki Meek Mill

0

WASHINGTON, MAREKANI

WEMA wa rapa kutokea nchini Marekani, Meek Mill umeonekana kumponza baada ya kujikuta katika kikaango cha mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki katika mitandao ya kijamii kwa kitendo chake cha kutoa dola 20 za kimarekani wagawane vijana sita waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza maji katika barabara za mitaa ya Atlanta.

Juzi, Rapper MeekMill alipost kipande cha video fupi akiwa anakatisha katika mitaa hiyo ya Atlanta, ndipo alipokutana na vijana wadogo wapatao sita waliokuwa wakizunguka barabarani wakiuza maji, akaingia mfukoni na kuwapatia vijana wale dola 20 za kimarekani ambazo zina thamani ya kama shilingi 48,000 za Kitanzania, akawaambia wagawane pesa hiyo kwa pamoja.

Huenda nia ya Meek Mill kuposti kipande kile cha video ilikuwa ni katika namna ya kuwahamasisha mastaa na watu wengine kurudisha kwa jamii, lakini katika hali ambayo rapa huyo hakuitarajia,  alijikuta akipokea kichapo cha maneno katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wengi wakihoji kwanini ametoa pesa kidogo kiasi kile licha ya yeye kuwa na uwezo wa kuwapa zaidi watoto wale watafutaji.

Posti moja kupitia ukurasa wa Twitter wa moja ya watu walioonekana kukerwa na kitendo hicho cha Meek Mill, “Sio wewe ambae unapiga kelele kuwaambia wenzako warudishe kwa jamii, umepata hiyo nafasi ya kurudisha kwa jamii na unatoa dollar 20 wagawane watu sita (6), huku gari ulilopanda lina thamani ya zaidi ya dola laki nne ($400,000), wewe ni kituko ambacho hakijawahi kutokea katika nchi hii.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here