Wema Sepetu: Naweza kuchanganyikiwa nikipata mtoto

0

Na Mwandishi Wetu

STAA wa filamu na msanii wa kike mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Wema Sepetu, amefunguka kuwa anaweza akachanganyikiwa kwa siku mbili au tatu endapo atapata mtoto wake.

Wema Sepetu alieleza hiyo kwenye ‘Insta Story’ yake baada ya kutoa fursa ya kuulizwa maswali 50 na mashabiki zake ambapo moja ya swali aliloulizwa ni kuhusu kupata mtoto wake ambapo amesema “Naweza kuchanganyikiwa kwa siku mbili au tatu naamini, hata mimi ningependelea hivyo ipo siku inshaalah”

Swali lingine aliloulizwa ni kitu anachojutia kwenye maisha yake ambapo Wema Sepetu akajibu kuwa kitu anachojutia ni kuamini watu kirahisi rahisi.

Huwezi kumzungumzia Wema bila kugusia muonekano aliokuwa nao baada ya kujipunguza ambapo kuhusu  hilo, alisema  “Unene ulikuwa haunifai kwenye ‘carrier’ yangu najipenda jinsi nilivyo kwa sasa”

Aidha, kupitia ‘Insta Story’ hiyo Wema ametusanua kuwa yupo kwenye mahusiano ‘serious’ na anatamani kuolewa na mtu kawaida ili kama kuchuma na kutengeneza basi watengeneze wote pia ampende kwa hali yoyote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here