WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA MAAGIZO MAZITO MFUMO WA USALAMA BANDARINI

0

*Waziri Mkuu Majaliwa afurahishwa na ujenzi wa Flomita Mpya.
*Aagiza Mifumo ya Usalama Ifungwe kudhibiti ubadhilifu na wizi wa wenye nia mbaya.
*Siku za Meli Kukaa Bandarini Zapungua, ataka zipungua zaidi

Na Merciful Munuo
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amepongeza maboresho yaliyopfanywa na mamlaka ya usimamizi wa bandari kwenye mitambo ya kushusha mafuta kwenye meli Flow Meters zilizop[o Bandari ya Dar es Salaam, na kuwataka wafanyakazi na Menejimenti ya TPA kusimamia weledi wa kazi kwani Bandari hiyo inategemewa kama chanzo kikuu cha mapato ya Serikali.

Waziri Mkuu ameyasema hayo kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kujenga mfumo wa kisasa wa ushushwaji wa mafuta melini FLOW METER, akikagua miundombinu hiyo iliyopo eneo la Kigamboni na Bandari ya Dar es Salaam.

“Nilivyokuja hapa mwaka 2016 teknolojia yetu lkuwa mbali sana, likuwa inatufanya tupoteze mafuta mengi na mapato mengi, lakini serikali yetu kuanzia Serikali ya awamu ya Nne ilifanya maboresho ya mitambo, na serikali ya awamu ya tano imetekeleza manunuzi ya mitambo ya kisasa, kutokana na kutoridhishwa na hali ilivyokuwa awali na sasa hali ni nzuri” Waziri Mkuu Majaliwa.

“Niliagiza kupatikane Viwanja na tujenge matanki yetu ya mafuta, nafurahi kuona viwannja vimenunuliwa na naagiza sasa tujenge matanki hayo ili wanaoleta mafuta yawekwe kwenye matanki yetu sio yanaenda moja kwa moja kwa mlaji, lazima tuwe na uhakika wa kila kitu tunachokifanya” Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu ameeleza kuwa mnamo mwaka 2016 alipotembelea eneo la bandari upande wa kuingiza mafuta alikuta mitambo ni michakavu jambo ambalo lilikuwa l;ikiingizia serikali hasara.

Waziri Mkuu Kassim majaliwa amewataka wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kuhakikisha kuwa wanakuwa waadilifu kwenye kuendesha mitambo ya Kisasa ya upakuaji wa mafuta kutoka melini Flow Meters za KOJ, Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, huku akiipongeza mamlaka ya usimamizi wa Bandari kwa kutekeleza maagizo ya serikali ya uboreshaji wa Mitambo hiyo.

Aidha Waziri Mkuu pia amewataka TPA kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha kwennye maeneo ya bandari kwani, kwa kufanya uharibifu au kupindisha muelekeo wa mafuta watu wenye nia mbaya wanaweza kusababisha hasara kwa serikali na upoteaji wa mapato.

“Niagize mfunge mitamb hii ya ufuatiliaji kwenye ofisi ya mkuu wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, pamoja na ofisi ya waziri wa ujenzi na uchukuzi na kwani kwa kufanya hivyo serikali itaweza kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu kama kuna uharibifu tukauliza na hatua zikachukuliwa, tusiruhusu viongozi wetu wa juu wakawa wanafuatilia kwa kuja kuja huku mara kwa mara, waone kwenye mifumo” Aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha waziri mkuu Majaliwa ameleza kuridhishwa na maboresho yaliyofanywa na TPA kufuatia maelekezo ya Serikali na kuwataka kufanya kazi usiku na mchana kwani eneo la bandari linategemewa na serikali kama chanzo cha mapato.

“Wafanya kazi wa bandari mfanye kazi ya usimamizi wa bandari kwani serikali inawategemea nyinyi, kwani hapa ndipo chanzo kikuu cha mapato ya serikali” Aliongeza waziri Mkuu Majaliwa.

Vilevile alieleza kuwa mamlaka ya usimamizi wa Banadari tanzania inatakuwa kuhakikisha kuwa foleni ya meli kukaa bandarini inapungua zaidi, kwani tayari wameweza kudhiibiti ushushaji wa meli za mafuta kutoka klukaa siku 15 hadi siku 8, ambapo mitambo hii mipya sasa itafanya mamlaka ya usimamizi wa bandari kushusha mafuta kwa siku chache zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here