Wawili wakutwa na corona Barcelona

0

MADRID, HISPANIA

KLABU ya Barcelona ya nchini Uhispania imethibitisha kuwa maafisa wake wawili wamekukutwa na COVID-19 usiku wa kuamkia jana (Januari 5, 2021), baada ya kufanyiwa vipimo kuelekea mchezo wao wa ligi kuu ‘La Liga’ dhidi ya Athletic Bilbao unaotaraji kuchezwa leo saa 5:00 usiku Januari 6.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa “Baada ya vipimo vya PCR vilivyofanywa jumatatu, maafisa wetu wawili kutoka kwenye timu ya wakubwa (ambayo ni Barcelona) walikutwa na COVID-19”.

“Klabu imewajulisha mamlaka husika za michezo na Afya, vilevile kikosi chote kitafanyiwa vipimo vya PCR zaidi siku ya Jumanne asubuhi leo (jana), kutokana na utaratibu mpya wa kujikinga na COVID-19”.

“Kutokana na hilo, muda wa kufanya mazoezi uliopangwa leo (jana), na zoezi la kuzungumza na wanahabari kuelekea kwenye mchezo wetu wa la liga dhidi ya Athletic Bilbao pia limeghairishwa na muda mwingine utapangwa kesho”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here