Wawili wahukumiwa jela miaka 18 shambulio la Westgate

0

NAIROBI, KENYA

MAHAKAMA nchini Kenya imewahukumu wanaume wawili kifungo cha miaka 18 jela, baada ya kuwakuta na hatia ya kulisaidia kundi la al-Shabaab kufanya mashambulizi kwenye duka la kifahari la Westgate mjini Nairobi. 

Watu 67 waliuawa katika mashambulizi hayo ya mwaka 2013. 

Waliopewa hukumu hiyo, Ahmed Abdi na Hussein Hassan Mustafa, kila mmoja amepatikana na hatia ya mashtaka mawili, na Abdi amepewa kifungo ziada cha miaka 15 kwa kupatikana na vifaa vya kueneza ugaidi. 

Mtuhumiwa wa tatu, Liban Abdullah Omar aliachiwa baada ya kuondolewa hatia wakati hukumu ya kesi hiyo iliposomwa Oktoba 7 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here