Watatu wafariki, 66 wakijeruhiwa ajali ya treni Dodoma

0

Na Mwandishi Wetu 

Taarifa za awali katika ajali ya treni iliyotikea eneo la Bahi inaonyesha watu watatu wamepoteza maisha.

Ajali hiyo imehusisha treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Kigoma na ilipata ilianguka ikiwa imepita vituo viwili vya Zuzu na Kigwe tangu ilipotoka kituo kikuu cha Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa eneo la tukio, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amesema miili mitatu ya wanawake iliopolewa katika behewa la pili.

“Hizo taarifa zinazozagaa sijui zinatoka wapi, sisi tuko eneo la tukio tukiendelea na kazi ya uokozi, nasema tumepata vifo vya watu watatu ambao wawili ni watu wazima na mtoto mdogo mmoja wote wa jinsia ya kike, “amesema Dk Mahenge.

Dk Mahenge amesema idadi ya majeruhi waliopelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma walikuwa 45 ambapo watatu kati yao walikuwa na hali mbaya lakini wengine wangeweza kutibiwa na kuruhusiwa kwani walikuwa wakijitambua.

Kuhusu manusura amesema taratibu zote zimefanyika na kulikiwa na mabasi ya kutosha kuwabeba na kuwapeleka Kituo cha Manyoni ambako wangeendelea na safari.

Aidha taarifa iliyotolewa na ShirIka la Reli Tanzania (TRC) imesema majeruhi waliongezeka na kufikia 66.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here