Watakaoandamana Dodoma kukutana na kipigo cha mbwa koko

0

Na Dotto Kwilasa, Dodoma 

Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amewasihi watu wanaotaka kuandamana waache kwa kuwa polisi wamejipanga kuwapa kipigo alichokiita cha mbwa koko.

Ameenda mbali zaidi na kudai wanaotaka kuandamana awali walishapata kipigo cha mbwa kachoka kwenye mchakato wa kura hivyo hawawezi kufanya lolote mtaani na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

RPC Muroto amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 2, 2020 jijini hapa katika mazoezi ya utayari yaliyofanywa na askari.

“Wamepigwa kipigo cha mbwa kachoka kwenye sanduku la kura sasa wanatangaza kuandamani. Sisi tutawapiga kipigo cha mbwa koko. Vikosi vyetu vipo kila sehemu,”amesema Muroto.

Hata hivyo, amesema bado hawajakamata watu kutokana na maandamano hayo.

Aidha,  amesema kuwa kama wanaona hawajatendewa haki kwenye uchaguzi mkuu wafuate taratibu nyingine za kisheria.

Wakati huohuo amesema jeshi limeimarisha ulinzi kuelekea siku ya kuapishwa rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Polisi wakiwa Katika mazoezi jijini Dodoma chini ya RPC Muroto

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here