Watahiniwa zaidi ya 600, 000 kufanya mitihani kidato cha pili

0

Na Mwandishi Wetu 

Watahiniwa 646,148 wamesajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa kidato cha pili unaotarajiwa kuanza kesho  Jumatatu Novemba 9 hadi Novemba 20, 2020.

Kati ya watahiniwa hao wavulana ni 301,831 sawa na asilimia 46.71 na wasichana  ni 344,317 sawa na asilimia 53.29.

Akizungumza leo Jumapili Novemba 8, 2020 katibu mtendaji wa  Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 5.7 ikilinganishwa na watahiniwa waliofanya mtihani huo mwaka 2019.

Amesema kati ya watahiniwa hao wapo wenye mahitaji maalum 731 wakiwemo 406 wenye uoni hafifu, 55 wasioona, 267 wenye ulemavu wa viungo na watatu wenye ulemavu wa kusikia.

Sanjari na kidato cha pili, katibu mtendaji huyo ameeleza kuhusu upimaji wa darasa la nne unaotarajiwa kufanyika Novemba 25 na 26, 2020.

Amesema wanafunzi 1,825,679 wamesajiliwa kufanya mtihani huo wa upimaji wakiwemo wavulana 909,068 na wasichana 916,611

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here