Home Uncategorized Wanyongwa kwa kosa la ubakaji

Wanyongwa kwa kosa la ubakaji

New Delhi, INDIA

Wanaume wanne nchini India waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la kumbaka mwanamke mmoja katika basi mnamo mwaka 2012 wamenyongwa leo Machi 20, 2020.

Adhabu hiyo imehitimisha kesi ambayo ilidhihirisha dhuluma ya kijinsia dhidi ya wanawake nchini India na kuwachochea raia wa nchi hiyo kudai haki kwa haraka zaidi.Wanaume hao walinyongwa katika gereza la Tihar la mji mkuu wa New Delhi.

Mwanamke  mwenye umri wa miaka 23, aliyekuwa mwanafunzi katika chuo cha Udaktari, alikuwa akitoka kuangalia sinema na rafiki yake wa kiume ndipo waliposhawishiwa na wanaume hao kupanda ndani ya basi hilo.

Walimuingilia mwanamke huyo kwa kutumia paipu ya chuma na alifariki wiki mbili baadaye kutokana na majeraha mabaya aliyoyapata.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments