Wananchi wa Kongwa wamshukuru JPM

0

NA DOTTO KWILASA,DODOMA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kongwa imemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuiwezesha wilaya hiyo kupata miradi mingi katika sekta ya afya na elimu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini hapa,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Dk Omari Nkullo alisema Halmashauri hiyo inamshukuru Rais Magufuli kwa kuipa miradi mingi katika sekta ya afya.

Alisema katika mwaka wa fedha 2019-2020 Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya sekta ya afya kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya,vituo vya afya pamoja na vifaa tiba.

Dk.Nkulo alisema katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa zimetolewa shilingi milioni 900 kwa ajili ya awamu mbili za ujenzi wa majengo.

Alisema pia wamejenga vituo vipya vya Mlali,Ugogoni na wanaendelea na ujenzi wa vituo vya afya vya Mbande na Mkoka.

“Rais wetu Dk.John Magufuli tunamshukuru kwani tumepokea fedha kwa ajili ya vituo vya Ugogoni shilingi milioni 400,

Mlali milioni 400,na tunaendelea na ujenzi kwa ajili ya kituo cha Afya cha Mbande Rais Dk Magufuli 2019 aliahidi kutoa mil 100 lakini ametoa mil 400 na ujenzi wake uko kwa asilimia 95,pia tumepokea mil 200 kwa ajili ya kituo cha Mkoka, “alisema Dk.Nkulo.

Alisema Zahanati 18 zimejengwa ikiwa ni pamoja na wodi za kina Mama na watoto hali ambayo imepunguza vifo vya mama na mtoto ambao wanafika kujifungua.

Hata hivyo alisema bado wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madaktari na wauguzi katika Halmashauri hiyo.

Vilevile,alisema wanakabiliwa na changamoto ya wananchi kutokujiunga katika mfumo wa bima ya afya,ambapo katika Kaya 60 ni Kaya 10 tu ambazo zimejiunga na mfuko huo.

Kuhusiana na elimu,Mkurugenzi huyo alimshukuru Rais kwa kuwapa Chuo kipya cha Ufundi Stadi (Veta) chenye majengo 13 ambayo tayari yamekamilika na yataanza kutumika hivi karibuni.

“Shule zetu zipo vizuri na tumekuwa tukiendelea kuzikarabati kwa kuhakikisha madawati yanapatikana na kunakuwa na walimu,”alisema .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here