Wamarakeni kuamua kati ya Trump na Biden

0

WASHINGTON, MAREKANI

Rais Donald Trump, amebakiza matarajio yake kwenye kura za moja kwa moja leo ili kutetea kiti chake na kuongoza kwa muhula wa pili baada ya mpinzani wake makamu wa Rais wa zamani, Joe Biden, kuongoza kura za mapema.

Leo Wamarekani wanamchagua Rais ingawa zaidi ya milioni 90 walishapiga kura za mapema kwa njia ya mtandao na posta na hesabu kuonyesha Biden anamzidi Trump.

Profesa kutoka Chuo Kikuu cha Florida, Michael McDonald jana alitoa ripoti iliyoonesha hadi Jumapili iliyopita, zaidi ya wananchi milioni 93.13 kutoka majimbo mbalimbali walifapiga kura.

Katika mgawanyo wa kura hizo, Profesa Mc Donald alisema milioni 34 zilipigwa kwa njia ya posta na milioni 59.12 kwa mtandao huku nyingine zaidi ya milioni 32.08 zilizopigwa kwa njia ya baruapepe zikiwa hazijahesabiwa.

Televisheni ya CNN inasema waliojitokeza kupiga kura mpaka sasa ni theluthi mbili ya waliopiga kura mwaka 2016 na inategemewa idadi itaongezeka zaidi kwani watu 239,247,182 wanaruhusiwa kufanya hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here