Walimu, wanafunzi VETA washikiliwa kwa rushwa

0

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera inawashikilia wanafunzi 38 wa chuo cha VETA Kagera na wakufunzi wao wawili, Francis Mwangosi na Ssenabulya Daud pamoja  pamoja na Mkuu wa Chuo hicho, Baluhi Mitinje kwa tuhuma za udanganyifu na rushwa kwenye chumba cha mtihani.

Aidha, taasisi hiyo pia inawashikilia wanafunzi 21 wa Chuo cha Tuinuane VTC na wakufunzi wao wawili, Charles Byabachwezi na Verdiana Myaka pamoja na Mkuu wa chuo hicho Emmanuel Jonas kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mitihani na matumizi mabaya ya ofisi kinyume na sheria.

Mkuu wa Takukuru mkoani Kagera, John Joseph amesema kuwa wanawashikilia wanafunzi hao pamoja na walimu wao kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika hao.

Sambamba na hilo, Mkuu huyo amesema kuwa wamekamata simu 38 zilizotumiwa na wanafunzi ndani ya vyumba vya mitihani wiki iliyopita pamoja na Sh 151,000/= zilizochangwa na wanafunzi kwenye mchakato wa kuwapatia wasimizi wa mitihani wa taifa wa elimu ya ufundi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here