Walimu Kenya wahofia afya yao huku shule zikifunguliwa

0

NAIROBI,KENYA

MAMILIONI ya watoto nchini Kenya wanarudi katika shule za msingi na zile za upili huku kukiwa na masharti yanayolenga kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Wanafunsi wa kidato cha nne wamekuwa wakiendelea na masomo yao tangu mwezi Oktoba lakini walichukua likizo fupi wakati wa likizo ya Disemba.

Baadhi ya wanafunzi katika shule za kibinafsi hatahivyo watalazimilka kusalia majumbani baada ya wamiliki wa shule hizo kuzibadilisha na kuzifanya maeneo ya biashara.

Hali hiyo inawalazimu wanafunzi waliokuwa katika shule zilizofungwa kutafuta maeneo mbadala.Cha kusikitisha ni kwamba wazazai wengi wana wasiwasi kuhusu hali ya usalama wa wanao huku wengi wakishindwa kutafuta karo na kununua vifaa vya kusomea.

Wengine wanalalamika kwamba kufungwa kwa sehemu nyingi za kufanyia kazi mbali na masharti makali ya kukabiliana na virusi vya corona yaliotolewa na serikali kumesababisha hali ngumu ya kiuchumi.

Waziri wa elimu Profesa George magoha amesimamia binfasi ufunguzi wa shule huku akitembelea shule mbali mbali jini Nairobi kuhakikisha kwamba hilo limeafikiwa .

Tayari Mkuu wa Muungano wa walimu nchini Kenya KNUT Wilson Sossion ameonyesha kutoridhishwa kwake kuhusu usalama wa wanfunzi na walimu huku shule nchini zikifunguliwa.

Sossion amesema kwamba maandalizi yaliopo kukabiliana na virusi vya corona hayatoshi katika mahojiano yake na kipindi cha redio cha BBC NewsDay.

Sossion amesema kwamba shule za siku ambazo ni nyingi zaidi ya zile za mabweni zitaathirika kwa kuwa nyingi hazina maji na luosha mikono.

Amesema kwamba serikali haijatoa fedha kwa shule kwa ununuzi wa vifaa vya kuwapima wanafunzi , vitakasa mikono ma vifaa vingine vinavyohitajika.

”Unapotoa ujumbe kama huo kwa shule na hujazipatia ufadhili …je watatekeleza vipi masharti hayo”.?

Wanafunzi katika shule za msingi na zile za upili walirudi shuleni siku ya Jumatatu.

Wizara ya elimu imetoa wito kwa walimu kutumia kila fursa ikiwemo kusoma chini ya miti ili kuweza kufuata sheria ya kutokaribiana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here