Wakala mwingine wa Chadema afariki

0

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ametangaza ongezeko kifo cha wakala mwingine wa chama hicho kilichotokana na ajali ya gari leo katika barabara ya Molo- Sumbawanga mkoani Rukwa. Awali iliripotiwa vifo vinne.

Wakala huyo alikuwa ni miongoni mwa majeruhi watatu ambao waliwahishwa hospitali mara baada ya ajali hiyo kutokea.

“Taarifa za awali zilitolewa kwamba mawakala wetu kule Sumbawanga wamefariki wanne, lakini mpaka sasa hivi majeruhi mmoja amefariki, kwahiyo wameongezeka na sasa jumla ya mawakala wa chama watano wamefariki”  amesema Mnyika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here