Wafanyabiashara watatu mbaroni kwa kusafirisha heroine kilo 3

0

Na Mwandishi Wetu

Wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha kilo 3.14 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Washitakiwa hao Abdallah Mpili, Haji Mustafa na Twalibu Kigesa maarufu kama Adebayo

Wakili wa Serikali Batilda Mushi, akisoma mashtaka ya watuhumiwa hao wa madawa ya kulevya mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Luboroga, alidai washitakiwa hao walitenda kosa hilo Oktoba, 2020 katika eneo la Azam Marine sehemu ya mizigo jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kuendesha kesi hiyo.

Na pia upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo imehairishwa hadi Novemba 10 itakapotajwa.

Washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here