Wafanyabiashara jela kwa kutaka kumpa rushwa DC

0
NA DOTTO KWILASA,DODOMA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoani Dodoma imewahukumu wafanyabiashara Nahid Bahadur Hirji na mwanaye Bahadur Hirji  kwenda Jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh milioni 1.5 baada ya kukiri mashtaka matatu ya kuahidi kutoa rushwa sh milion 1.2 kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi.
Washtakiwa hao wamekutwa na adhabu hiyo baada ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani hapa TAKUKURU kuwabaini washtakiwa hao mwaka jana wakifanya jinai hiyo kutenda kitendo hicho ambacho ni kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkuu wa Takukuru Dodoma Sosthenes Kibwengo alisema kitendo walichofanya wafanyabiashara hao ni kinyume na kifungu cha sheria cha kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007.
Kibwengo alisema Takukuru Dodoma iliwafikisha mahakamani washtakiwa hao baada ya uchunguzi kukamilika iliwafikisha mahakamani kutokana na mgogoro wao wa kifamilia.
Alisema hiyo iwe fundisho kwa jamii na familia ambazo zinamigoro kuacha kupita njia za panya.
Katika hatua nyingine Takukuru imefanikiwa kumrejeshea Mwalimu mstaafu Stanley Godfrey Matonya sh milioni 22.4 alizodhulumiwa na kampuni ya Kabugama CO. LTD ya jijini hapa tangu 2016 ambazo alitoa kwa lengo la kupatiwa trekta.
Kibwengo alisema Mwalimu huyo alitakiwa kupewa trekta aina Swarrag 744 lenye jembe moja pamoja na tela kwa maelewano ya kulipa sh milion 23.9 ambayo ni ssilimia 50 kulingana na mkataba waliokubaliana.
Hata hivyo katika kufuatilia ndani ya miaka minne alifanikiwa kurudishiwa sh milion 1.5.
Kibwengo alisema uchunguzi wao ulikamilika na kubaini ubadhilifu na kuiamuru kampuni hiyo kumrejeshea sh milion 22.4 alizokuwa anawadai.
Mbali na huyo pia wamefanikiwa kumrejeshea Ahmed Talibu mkazi wa jijini hapa sh milion 6.4 za kiwanja ambacho kimepitiwa na mradi wa reli.
Kibwengo alisema fedha hizo ni malipo ya fidia ambayo alipewa Noorjan Ahmed aliyeuziwa kiwanja kitapeli na watuhumiwa ambao wanaendelea kutafutwa ili wafikishwe mahakamani.
Naye Talibu aliishkuru Takukuru kutokana na msaada inayotoa kwa wananchi wanaodhumiwa haki zao.
Alisema watu wasisite kwenda Takukuru kama wanavigezo vyote ili kufuatilia haki zao.
Kwa upande wa mwalimu mstaafu Matonya alisema ameteseka kwa muda mrefu hivyo Takukuru ndio imekuwa mkombozi wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here