Wadau wa michezo Zanzibar wampongeza Rais Hussein Mwinyi

0

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

WADAU wa Soka Visiwani Zanzibar wamempongeza Rais Mteule Dk. Hussein Ali Mwinyi, huku wakiwa na matumaini makubwa kwa michezo kupiga hatua, wakimuomba kutekeleza ahadi zake za kimichezo alizoahidi wakati wa kampeni.

Ikumbukwe kuwa Oktoba 15 mwaka huu, Dk. Mwinyi alikutana na wanamichezo Visiwani humo huku akiwaahidi kuwa pindi wananchi watakapompa ridhaa ya kuongoza nchi, michezo itapiga hatua.

Mmoja wa wadau hao wa michezo, Samit Hadhir Mohamed, alisema amefurahi kwa kupata rais wao waliomchagua  na wanatarajia mabadiliko makubwa katika sekta ya michezo.

“Kwa sababu rais wetu ni kijana maana sio kizee hajazeeka bado, ni kijana na pia ataleta maendeleo kiufupi katika jamii yetu hii na hasa kwenye sekta ya mchezo zaidi,”alisema Mohamed.

Aidha, Wadau hao, walisema wamefarijika mno Dk. Mwinyi kupata nafasi hiyo ya urais kwa sababu yeye kama yeye amejikita katika kusimamia masuala ya vijana hususan katika masuala ya michezo.

“Naamini kwamba michezo itakuwa kupitia Dk. Husssein na kila kitu ambacho kinaekwa ahadi kitafanyiwa kazi, natumai kwamba michezo itakuwa na itapiga hatua.

“Aliwahi kukutana na sisi wanamichezo na aliahidi kwamba masuala ya michezo atayafanyia kazi na ataweza kutupa kipaumbele wanamichezo, naamini kwamba ahadi zake ataweza kuzifanyia kazi,”alisema mmoja wa wadau hao.

Walisema kwa vile viajana wengi wamejikita kwenye mchezo wa mpira wa miguu wakiaamini kuwa ndio ajira iliyopo kwa sasa hivyo alimuomba awaboreshee viwanja.

Oktoba 15 wakati wa kampeni Dk Mwinyi alikutana na wanamichezo Visiwani humo na aliwaahidi kuwa pindi atakapokuwa Rais michezo itapiga hatua.

“Michezo lazima iwezeshwe, rasmali fedha ni muhimu kataika michezo hakuna njia nyingine hatuwezi kusema tutakuwa na uongozi bora, tukawa na hiki na hiki kama hatutazungumzia fedha michezo haiwezi kwenda mbele.

“Lazima tutafute njia ya kupata fedha na njia ziko nyingi kwa tatu, moja Serikali iweke fungu maalumu la michezo.

“Pili udhamini lazima sekta binafsi ishirikishwe katika maendeleo ya michezo na tatu ni kwa upande wa vyama vyewe kukutana watu kukubali fedha zao kuingia kwenye michezo, fedha zile zitumike vizuri.

“Tuna vingi katika nchi yetu, vyama vimichezo vyote fedha ni muhimu, ninaomba tuhakikishe kwamba maeneo haya matatu, sasa mimi ombi langu ni hili.

“Niwe na Serikali mwenyezi Mungu akinijalia lakini mimi nitawatafuta wadhamini, lazima watu wote wanaofanyabiashara hapa Zanzibar awe tayari kudhamini michezo,”alisema Dk. Mwinyi wakati alipokutana na wanamichezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here